Na Bora Mustafa, Arusha.
Msaada huo ni mwendelezo wa misaada ya kusaidia jamii ambayo imekuwa ikitolewa na Chem Chem wilayani Babati katika sekta ya Afya,Elimu,Maji na huduma nyingine za kijamii.
Akizungumza Machi 29, 2026 wakati wa kukabidhi viti hivyo, Meneja Mkuu wa Chem Chem, Clever Zulu amesema wanapongeza shirika la Chair The Love la Marekani kuendelea kushirikiana na Chem Chem katika kusaidia jamii.
Zulu amewataka wananchi waliopo katika vijiji 10 ambavyo vinaunda hifadhi ya wanyamapori ya jamii ya Burunge, eneo ambalo taasisi hiyo imewekeza kuendelea kutunza mazingira na wanyamapori ili kuendelea kuvutia watalii zaidi.
Meneja Miradi ya maendeleo ya jamii wa Chem Chem ,Napendael Wazoeli amesema Lengo la Chem Chem nikuisaidia Jamii kupitia uhifadhi ambao umeendelea kuwanufaisha Wananchi ambao wapo pembezoni mwa hifadhi.
Wazoeli amesema , msaada huo ni sehemu ya matunda ya uhifadhi wa mazingira na wanyamapori katika wilaya hiyo ambayo Chem Chem imewekeza Utalii wa picha na hoteli.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Babati , Mwanasheria wa Halmashauri hiyo Jofrey Jaffar amewataka Jamii kuendelea kuunga Mkono Taasisi ya Chem Chem ambayo imewekeza katika wilaya hiyo ili kuendelea kunufaika.
Aidha Jaffar amesema taasisi ambazo zimeweleza katika eneo hilo la Burunge WMA zimekuwa zinaigusa jamii moja kwa moja kupitia misaada inayotolewa.
Pia Baadhi ya wananchi waliopokea msaada huo wameishukuru Taasisi ya Chem Chem na washirika wake kwa msaada huo ambao utarahisisha maisha yao.
Rehema Peter mkazi wa kijiji cha Vilima vitatu moja ya vijiji 10 vinavyounda hifadhi hiyo aliomba Taasisi hizo kuendelea kutoa msaada kwa wahitaji ambao bado hawajafikiwa kwa njia moja ama nyingine.
Msaada huo umetolewa kwa mwaka wa nne sasa na Taasisi ya Chem Chem kwa ushirikiano na Shirika la Chair The Love kutoka nchini Marekani ambao wameahidi kuendelea kusaidia kwenye maeneo mbalimbali hapa Nchini.









Social Plugin