Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ZIARA YA DC KISHAPU YAACHA KICHEKO KWA WAKULIMA WA PAMBA

Na Sumai Salum-Kishapu

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Peter Masindi, Februari 18, 2026 ametembelea Kata za Mwamashele na Lagana kwa lengo la kufuatilia kwa karibu maendeleo ya zao la pamba, hali ya nyenzo za upuliziaji sumu pamoja na ugawaji wa vifaa vya pembejeo kwa wakulima waliokidhi vigezo.


Katika ziara hiyo iliyojaa hamasa na matumaini mengi kwa wakulima, Mhe. Masindi amesisitiza umuhimu wa kuzingatia kanuni za kilimo bora ikiwemo upandaji kwa mistari, matumizi sahihi ya viuatilifu pamoja na ufuatiliaji wa karibu wa mashamba ili kuongeza tija na mavuno yenye ubora.


Akiwahimiza wakulima kuongeza uzalishaji, amesema Serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha mkulima wa pamba anainuliwa kiuchumi kupitia uwezeshaji wa pembejeo na usimamizi wa kitaalamu wa kilimo.


“Watumieni vijana wa BBT ili kuwa na kilimo chenye tija na chenye matokeo chanya. Ushirikishwaji wao utaongeza nguvu kazi na maarifa mashambani,” amesisitiza Mhe. Masindi.


Ameongeza kuwa ugawaji wa vifaa vya pembejeo unalenga kuwafikia wakulima wanaozingatia kanuni za kilimo bora, ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha uwekezaji wa Serikali unazaa matokeo yenye manufaa kwa mkulima mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Peter Masindi, akizungumza na baadhi ya wakulima wa zao la pamba Kata ya Mwamashele wilayani humo kwenye ziara yake kwenye Kata hiyo na Kata ya Lagana yenye lengo la kufuatilia kwa karibu maendeleo ya zao la pamba, hali ya nyenzo za upuliziaji sumu pamoja na ugawaji wa vifaa vya pembejeo kwa wakulima waliokidhi vigezo Februari 18,2026


Kwa upande wake, Mkaguzi wa zao la Pamba wilayani humo, Joachimu John Gabanya akizungumza wakati wa ziara hiyo, amewataka wakulima kutunza vifaa walivyopokea na kuvitumia kwa uangalifu ili viendelee kuwasaidia kwa muda mrefu na kuongeza ufanisi katika uzalishaji.


Miongoni mwa wakulima walionufaika na ziara hiyo ni Juma Paul Njile, mkulima mwenye ekari 37 kutoka Kata ya Mwamashele, ambaye ameeleza mafanikio aliyoyapata kupitia kilimo cha pamba kinachofuata misingi sahihi ya kitaalamu.


“Miaka ya nyuma nilifanya majaribio ili kubaini kama tunachoambiwa na wataalamu ni sahihi kuhusu ubovu wa mazao mseto, hivyo niliamua kulima shamba mseto moja na lingine sikulichanganyia zao jingine bali pamba peke yake kwenye lile shamba mseto nilipata mavuno machache, lakini lile nililolima kwa kufuata kanuni za kilimo bora, niliona faida kubwa. Kilimo hiki kinalipa. Msimu huu wa 2026/2027 natarajia kuvuna kilo 3,700,” amesema kwa kujiamini.


Sambamba na hilo, Mkuu wa Wilaya ameshuhudia matumizi ya nyenzo za upuliziaji sumu katika baadhi ya mashamba na kugawa jumla ya vifaa vya pembejeo aina ya Solo pump 19 kwa wakulima waliokidhi vigezo katika Kijiji cha Mihama, Kata ya Lagana ikiwa ni miongoni mwa solo pump 1000 zilizopokelewa Wilayani humo.


Ziara hiyo imeacha alama ya matumaini, ikionyesha dhamira ya Serikali ya kuimarisha zao la pamba kama mhimili muhimu wa uchumi wa wakulima na Taifa kwa ujumla.
Mkaguzi wa zao la Pamba wilayani Kishapu mkoani Shinyanga kutokea Bodi ya pamba mkoani Mwanza Joachimu John Gabanya, akizungumza kwenye ziara ya Mkuu wa Wilaya hiyo Kata ya Mwamashele na Lagana yenye lengo la kufuatilia kwa karibu maendeleo ya zao la pamba, hali ya nyenzo za upuliziaji sumu pamoja na ugawaji wa vifaa vya pembejeo kwa wakulima waliokidhi vigezo Februari 18,2026Afisa Tarafa ya Negezi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Tano Malele, akizungumza kwenye ziara ya Mkuu wa Wilaya hiyo Kata ya Mwamashele na Lagana yenye lengo la kufuatilia kwa karibu maendeleo ya zao la pamba, hali ya nyenzo za upuliziaji sumu pamoja na ugawaji wa vifaa vya pembejeo kwa wakulima waliokidhi vigezo Februari 18,2026Diwani wa Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Lucas Daudi Nkende, akizungumza kwenye ziara ya Mkuu wa Wilaya hiyo Kata ya Mwamashele na Lagana yenye lengo la kufuatilia kwa karibu maendeleo ya zao la pamba, hali ya nyenzo za upuliziaji sumu pamoja na ugawaji wa vifaa vya pembejeo kwa wakulima waliokidhi vigezo Februari 18,2026Afisa kilimo Bodi ya pamba kutokea mkoani Mwanza Edward Nyawile, akizungumza kwenye ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Peter Masindi Kata ya Mwamashele na Lagana yenye lengo la kufuatilia kwa karibu maendeleo ya zao la pamba, hali ya nyenzo za upuliziaji sumu pamoja na ugawaji wa vifaa vya pembejeo kwa wakulima waliokidhi vigezo Februari 18,2026Mratibu wa zao la Pamba Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Richard Manguha, akizungumza kwenye ziara ya Mkuu wa Wilaya hiyo Kata ya Mwamashele na Lagana yenye lengo la kufuatilia kwa karibu maendeleo ya zao la pamba, hali ya nyenzo za upuliziaji sumu pamoja na ugawaji wa vifaa vya pembejeo kwa wakulima waliokidhi vigezo Februari 18,2026


















Muonekano wa shamba la pamba ambalo halijachanganywa na mazao mengine

Mfano Shamba lililopandwa mazao mseto linalopelekea kuababisha kupunguza ubora wa mazao na kupelekea uchache wa mavuno
































Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com