Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SPIKA ZUNGU ASEMA HAKUNA MBUNGE ALIYEPEWA KIBALI KUHOJIWA NA TAKUKURU



Na mwandishi wetu, Dodoma

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu, amesema hadi sasa Ofisi ya Spika haijatoa kibali chochote kwa mbunge yeyote kuhojiwa na TAKUKURU. 

Hii ni kufuatia taarifa za vyombo vya habari zikidai baadhi ya wabunge wameitwa kuhojiwa kuhusiana na madai waliyoyatoa bungeni jambo ambalo Spika amekanusha.

Spika amesisitiza kuwa Bunge linaongozwa na Katiba na Kanuni zake, zinazolinda uhuru wa wabunge kutoa maoni bila shinikizo, hofu au kikwazo chochote. Uhuru huu umeainishwa na Ibara ya 100 ya Katiba, ikiwapa wabunge kinga ya kisheria.

Ameongeza kuwa endapo mbunge amekiuka Kanuni, mamlaka ya kuchukua hatua ipo ndani ya Bunge lenyewe kupitia Kiti cha Spika. Bunge litaendelea kulinda uhuru wa wabunge kuchangia masuala ya kitaifa kwa uwazi na ujasiri.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com