
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea nakala ya kitabu "Jamhuri ya Plato" kilichotafsiriwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutoka kwa Bw. Walter Bgoya, Mkurugenzi wa kampuni ya uchapishaji ya Mkuki na Nyota, jijini Dar es Salaam.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea nakala ya vitabu vya wasifu na hotuba vya Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin William Mkapa
**
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amepokea nakala ya kitabu Jamhuri ya Plato, kilichotafsiriwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kutoka kwa Bw. Walter Bgoya, Mkurugenzi wa kampuni ya uchapishaji ya Mkuki na Nyota, mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
Kitabu hicho, ambacho asili yake ni The Republic (Politeia) cha mwanafalsafa wa Kigiriki Plato, kinaangazia mazungumzo ya Socrates, ambapo Plato anachambua aina mbalimbali za tawala, asili ya nafsi, nadharia ya maumbo pamoja na dhana ya mji bora (Kallipolis) unaoongozwa na wanafalsafa-wafalme.
Tafsiri ya Mwalimu Nyerere inaleta fikra hizo katika muktadha wa Afrika, kwa kusisitiza umuhimu wa maadili, uongozi wenye hekima na wajibu wa raia katika kujenga jamii bora na yenye haki.
Social Plugin