Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

POLISI YACHUKUA HATUA KWA MATUKIO MATATU YA VIFO, LIPO LA ALIYEJINYONGA MAHABUSU



Na Mwandishi wetu, Dar

Jeshi la Polisi limetangaza kumshikilia askari mmoja wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji kwa tuhuma za kumpiga risasi Shaban Said Luluba, Mkazi wa Kijiji cha Nyamwage Wilayani Rufiji na kupelekea kupoteza maisha wakati akifanya ukamataji Januari 08, 2025.

Taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya habari na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania

Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Misime imesema Uchunguzi unaendelea kuhusu tukio hilo na endapo itabainika kuna uzembe au matumizi zaidi ya nguvu hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa dhidi ya askari huyo.

Misime pia amesema Jeshi hilo linafanya uchunguzi wa matukio ya vifo vilivyotokea kwa nyakati tofauti Tarime/Rorya pamoja na Jijini Arusha ikiwemo tukio la kifo cha Dickson Tadeus Joseph, mkazi wa Rebu Senta Wilayani Tarime kilichotokea Januari 01, 2026 huko katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime.

"Baada ya kutokea kifo hicho, Jeshi la Polisi limepokea barua ya malalamiko kuwa, kifo hicho hakikutokana na Dickson Tadeus Joseph (marehemu) kuanguka katika eneo la Mtaa wa Serengeti wakati akikimbia kama ilivyo elezwa awali bali kimesabababishwa na Askari Polisi." Amesema Misime.

Kulingana na Polisi, uchunguzi wa kina umeanza kuhusu tukio hilo na kulingana na ushahidi kutoka kwa watu walioshuhudia, ikibainika kuna Askari aliyehusika hatua stahiki kwa mujibu wa sheria zitachukuliwa dhidi yake.

Misime amezungumzia pia taarifa ya Viollete Uwumuhoza, Raia wa Rwanda ambaye alijinyonga Januari 07, 2026 akiwa mahabusu ya Polisi Jijini Arusha, alikokuwa akishiliwa kwa kosa la kuingia na kuishi nchini kinyume cha Sheria ambapo uchunguzi wa kina unaohusisha uchunguzi wa kisayansi na wa haraka unaendelea kuhusiana na tukio hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com