Na Mwandishi wetu, Dar
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, leo tarehe 02 Januari 2026 amemtembelea na kumjulia hali Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal, katika makazi yake yaliyopo Masaki jijini Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo ya heshima na utu, Dkt. Nchimbi ameeleza dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuendelea kuthamini mchango wa viongozi wastaafu katika ujenzi wa Taifa, akisisitiza kuwa uzoefu na busara zao ni hazina muhimu kwa maendeleo ya nchi.
Kwa upande wake, Dkt. Gharib Bilal amemshukuru Makamu wa Rais kwa kumtembelea, akieleza kufarijika na kuendelea kwa mshikamano na mawasiliano kati ya viongozi walioko madarakani na wale waliotumikia Taifa katika vipindi tofauti.
Ziara hiyo imeendelea kudhihirisha utamaduni wa kuheshimiana, kuthaminiana na kudumisha umoja wa kitaifa, sambamba na kuimarisha misingi ya maadili na uongozi bora nchini.



Social Plugin