Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KATIBU MKUU WA NLD AONGOZA KIKAO CHA TATHIMINI YA UCHAGUZI WA MWAKA 2025

 


Na Mwandishi Wetu,DAR

KATIBU MKUU wa Taifa wa Chama cha NLD Doyo Hassan Doyo January 6 mwaka huu ameongoza kikao cha Tathimini ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba mwaka 2025 cha Watendaji wa Makao Makuu na Afisi Kuu pamoja na Wagombea Wote.

Wagombea hao ni waliogombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo, ikiwa ni maandalizi ya vikao vya kikatiba vinavyotarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.

Katika kikao hicho kimepitisha pia Taarifa ya maandalizi ya kugombea Ubunge Jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma wakati tume itapotangaza rasmi kuanza mchakato wa kumpata mwakilishi wa Jimbo hilo .

Katibu Mkuu huyo aliwashukuru  wananchi wote waliokiunga mkono chama chetu katika kampeni zake nchin kote wakati wa uchaguzi mkuu.

Hata hivyo alitumia nafasi hiyo kuwashukuru  wagombea wote waliogombea nafasi mbalimbali kote nchini nakuwataka wasife moyo na kujipanga kisawasawa katika chaguzi zijazo katika nchi yetu kwani hiyo ndyo njia pekee ya kuweza kushika Dola.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com