Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DIWANI SHABANI RASHIDI AKAGUA BARABARA BAKOBA, AWEKA MSINGI WA MATENGENEZO YA DHARURA NA BAJETI IJAYO

Na Mbuke Shilagi Kagera.

Diwani wa Kata ya Bakoba, Mhe. Shabani Rashidi, amefanya ziara ya kikazi katika maeneo mbalimbali ya kata hiyo akiwa pamoja na Maofisa kutoka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Bukoba, kwa lengo la kukagua hali ya barabara na kubaini maeneo yenye uharibifu mkubwa yanayohitaji matengenezo ya dharura.
Ziara hiyo imelenga pia kuainisha vipaumbele vitakavyoingizwa katika maandalizi ya bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027, ili kuboresha miundombinu ya barabara kwa manufaa ya wananchi wa Kata ya Bakoba na Manispaa ya Bukoba kwa ujumla.

Katika ziara hiyo, barabara muhimu zilizokaguliwa ni pamoja na Bishop Road/Gholani Street, Ukerewe Road na Shelisheli Road ambazo Barabara hizo ni mhimili mkubwa wa shughuli za kiuchumi, kijamii na usafiri, hivyo uboreshaji wake unatarajiwa kuongeza usalama na kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Shabani Rashidi amesema kuwa dhamira ya uongozi wake ni kuhakikisha changamoto za miundombinu zinashughulikiwa kwa vitendo kupitia ushirikiano wa karibu na taasisi za Serikali pamoja na ushirikishwaji wa wananchi.

Kupitia ushirikiano kati ya Ofisi ya Diwani na TARURA Bukoba, maeneo korofi yameainishwa kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo ya haraka, sambamba na kuyaingiza katika mipango ya muda mrefu kupitia bajeti ijayo,Hatua ambayo inalenga kuboresha usafiri, usalama wa wananchi na mazingira ya biashara katika Kata ya Bakoba.

Uongozi wa Mhe. Shabani Rashidi unaendelea kujengwa juu ya misingi ya uwajibikaji, uwazi na matokeo, huku akisisitiza kuwa maendeleo ya Bakoba yataendelea kuwa kipaumbele chake cha msingi.










Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com