Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANANCHI WA JIMBO LA NGARA WAHIMIZWA KUJITOKEZA KWENYE VITUO WALIVYOJIANDIKISHIA KWA AJILI YA KUPIGA KURA OCTOBER 29



Mgombea Ubunge Jimbo la Ngara Dotto Jasson Bahemu akiwaonyesha wananchi mfano wa karatasi ya kupigia kura
Wananchi wa Jimbo la Ngara kata ya Bukiriro wakiwa kwenye mkutano wa mgombea Ubunge Dotto Jasson Bahemu

‎Na Mariam Kaagenda _Kagera

Mgombea Ubunge wa  Jimbo la Ngara Dotto Jasson Bahemu  amewataka Wananchi  wa Jimbo hilo wenye sifa za kupiga kura kujitokeze kwa wingi  tarehe 29 Oktoba, 2025 kumchagua Rais, Mbunge na Madiwani
Akizungumza na Wananchi katika mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Kata ya Bukiriro, mgombea huyo wa Ubunge ameomba kura za Mgombea Udiwani  kupitia Chama Cha Mapinduzi Bwana Erick Emily Nkilamachumu, kura za Mbunge Dotto Jasson Bahemu na Kura za mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

Bahemu amesema kuwa zoezi la upigaji wa kura ni haki kwa kila Mtanzania mwenye sifa za kupiga kura hivyo  wananchi wa Jimbo la Ngara wanatakiwa kujitokeza kwa wingi katika vituo vya kupigia kura walivyojiandikishia ili kutimiza haki yao.

  Akiomba kura za Mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bahemu amesema katika kipindi cha Miaka 4 Rais Samia amefanya mambo mengi ya maendeleo kupitia miradi iliyogharimu takribani kiasi cha shilingi  bilioni 81.

‎‎Aidha, amewataka Wananchi wote kuhakikisha wanapiga kura za ndiyo kwa wagombea wote wa Chama Cha Mapinduzi ili waweze kuharakisha maendeleo ya Jimbo hilo





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com