Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CHATANDA AWAHAMASISHA WANAKIGAMBONI OKTOBA 29, 2025 KWENDA KUPIGA KURA NA KUMCHAGUA DKT. SAMIA




Mwenyekiti wa UWT Taifa, Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) ameambatana na Katibu Mkuu wa UWT Taifa, Ndg. Suzan Peter Kunambi (MNEC) leo 18 Oktoba, 2025, katika Viwanja vya Tungi Mnadani, Wilaya ya Kigamboni na amewaomba wananchi wa Kigamboni kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la kupiga kura Oktoba 29, 2025.

Aidha amewaomba kuhakikisha wanapiga kura kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na wagombea wa Ubunge na Udiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Chatanda amewahimiza wananchi, hususani vijana wa Jimbo la Kigamboni, kutobabaishwa na Wagombea Wengine kwasababu Dkt. Samia amejipambanua kwa Kazi zake.

 Kauli hiyo aliitoa wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kushiriki Bonanza la Mazoezi ya Kutembea (Jogging) na Michezo Mbalimbali lililoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Ndg. Dalmia Mikaya.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com