
Katika maziko hayo yaliyofanyika jana Oktoba 13/2025 katika makaburi ya kijamii yaliyopo kata ya Hasanga wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, Dini wazee maarufu na raia wa kawaida walishiriki maziko hayo.
Imeelezwa kuwa chanzo cha kifo hicho ni mtoto huyo kudonolewa na kuku mara baada ya kutoka kwenye sherehe za kuhitimu darasa la saba siku za hivi karibuni na kusababisha kifo chake baada ya jitihada za matibabu na maombi kushindikana.
Baba mzazi wa mtoto huyo, Benjamin Makelo katika maziko hayo alishindwa kujizuia baada ya kushindwa kusimama akisaidiwa na ndugu kumuinua katika kaburi hilo la mwanae.
Raphael Mtafya kiongozi wa mtaa na mwimbaji wa kwaya katika kanisa alilokuwa akisali marehemu huyo, amesema kifo hicho kimejawa na mshangao mkubwa kutokana na kudonolewa na kuku usiku wa saa nane.
Amesema alipotoka kupokea zawadi kwenye sherehe hizo za kuhitimu darasa la saba usiku wakati amelala aliota ndoto kuwa amedonolewa na kuku aliposhituka alimueleza baba yake juu ya ndoto hiyo.
“Siku iliyofuata saa saba usiku alishituka kitandani baada ya kuku aliyemuota kumjia na kumdonoa katika paji la uso na ilipofika asubuhi alianza kuugulia maumivu makali.
“Baada ya maumivu hayo kuzidi alipelekwa hospitali ya wilaya iliyopo Vwawa na kufanyiwa vipimo ambavyo havikuonesha ugonjwa na ndipo walipompeleka kanisani kufanyiwa maombezi,” amesema.
Mtafya ambaye pia ni balozi wa nyumba kumi katika mtaa huo, amesema kuwa baada ya homa kuzidi wakampeleka hospitali ya Rufaa mkoani Songwe ambako nako vipimo havikuonesha ugonjwa.Aidha, ameeleza kuwa baada ya hapo marehemu alirejeshwa nyumbani na alizidi kuumia huku jicho moja likiziba na alianza kuharisha mfululizo na ilipofika usiku wa saa nane ya kuamkia juzi alifariki dunia na amezikwa Oktoba 13,2025.
“Mimi ni shemansi wa kanisa na ni balozi wa mtaa shina namba 2, baba wa mtoto ni Mwalimu wa sande, mtoto alikuwa mwimbaji na mwenye kuijua vyema bibilia, tulijaribu kumuombea lakini ilishindakana, kifo chake kimewashangaza wengi,” amesema Mtafya.
Mwenyekiti wa mtaa wa Maejengo Leonard Mwambene amesema ameshiriki maziko hayo huku akijiuliza chanzo cha kifo hicho na kuwa yote hayo ni mipango ya Mungu.
Amesema tukio hilo ni la kusikitisha na halijawahi kutokea katika mtaa wake,akishangazwa kuku ambaye hana vifaranga kusababisha kifo cha mtu huku akiwaasa wazazi kutojichanganya Pamoja na mifugo ili kuepukana hatari kama hii iliyojitokeza kwa mtoto Josiah.
Afisa mtendaji wa kata ya Hasanga Frola Ndamu licha ya kukiri kuwepo na tukio hilo, amesema hizo ni kazi za MUNGU kwani akipangacho hakuna binadamu anayeweza kuzuia.
Kamanda wa polisi mkoani Songwe Augustino Senga, amesema suala hilo bado halijafika mezani kwake.
Social Plugin