Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : KATAMBI AHITIMISHA KAMPENI KWA KISHINDO SHINYANGA MJINI, AWAOMBA WANANCHI KUPIGIA KURA WAGOMBEA WA CCM KWA WINGI OKTOBA 29

Mgombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, akinadi Ilani ya CCM kwenye mkutano wa kufunga kampeni uliofanyika katika viwanja vya Relini, Kata ya Mjini, Shinyanga, Oktoba 25, 2025.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 Blog

Mgombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, leo Jumamosi Oktoba 25, 2025 amehitimisha kampeni zake za uchaguzi mkuu kwa mkutano mkubwa katika viwanja vya Relini, Kata ya Mjini, Shinyanga.

Akizungumza wakati wa kufunga kampeni, Katambi amewataka wananchi wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi Oktoba 29, 2025 kupiga kura kwa Amani na Utulivu, na kuwachagua wagombea wote wa CCM kuanzia ngazi ya Udiwani, Ubunge hadi Urais.

“Tuendelee kuipa kura CCM, chama chenye dira, uadilifu na matokeo chanya. Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ameleta mageuzi makubwa katika uchumi, elimu, maji, na miundombinu. Ni jukumu letu kumuunga mkono kwa vitendo kupitia sanduku la kura,” amesema Katambi huku akishangiliwa na wananchi.

Katambi pia ametoa wito kwa wananchi kuepuka maneno ya uchochezi, chuki, na vurugu kipindi cha uchaguzi, akisisitiza kuwa amani ni msingi wa maendeleo.

“Tunataka ushindani wa hoja, siyo fujo. Shinyanga tumejipanga kushinda kwa amani na kwa hoja,” ameongeza Katambi.

Katika mkutano huo wa kufunga kampeni, viongozi mbalimbali wa CCM, wagombea wa Udiwani, na wanachama wa chama hicho wamehudhuria huku burudani mbalimbali  zikiongeza hamasa kwa umati wa wananchi.

Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unatarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025, ambapo wananchi watachagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge, na Madiwani kote nchini.
Mgombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, akinadi Ilani ya CCM kwenye mkutano wa kufunga kampeni uliofanyika katika viwanja vya Relini, Kata ya Mjini, Shinyanga, Oktoba 25, 2025. Picha na Malunde 1 blog
Mgombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, akinadi Ilani ya CCM kwenye mkutano wa kufunga kampeni uliofanyika katika viwanja vya Relini, Kata ya Mjini, Shinyanga, Oktoba 25, 2025.
Mgombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, akinadi Ilani ya CCM kwenye mkutano wa kufunga kampeni uliofanyika katika viwanja vya Relini, Kata ya Mjini, Shinyanga, Oktoba 25, 2025.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com