Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAHAFALI YA 19 YA DARASA LA SABA HOPE ENGLISH MEDIUM PRIMARY SCHOOL YAFANYIKA SHINYANGA


Shule ya Msingi Hope English Medium Primary School iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga imefanya mahafali ya 19 ya darasa la saba, tukio lililohudhuriwa na wazazi, walimu na wageni waalikwa.

Katika mahafali hayo yaliyofanyika Septemba 19, 2025 wazazi na walezi wamekumbushwa umuhimu wa malezi bora ya watoto yanayojenga heshima na sifa njema kwa jamii. Imeelezwa kuwa changamoto ya matumizi makubwa ya simu miongoni mwa wazazi imekuwa ikipunguza nafasi ya watoto kupata simulizi na mafunzo ya kitamaduni kutoka kwao.

Aidha, shule hiyo imewaomba wazazi na walezi wa Shinyanga kutopeleka watoto wao mbali na nyumbani kwa ajili ya masomo, kwani hali hiyo huongeza gharama na changamoto pindi mtoto anapokutana na mazingira mapya. Shule imeahidi kuendelea kutoa elimu bora katika mazingira rafiki na salama kwa watoto.

Mahafali hayo pia yalipambwa na burudani mbalimbali za wanafunzi pamoja na pongezi kwa wahitimu wa darasa la saba mwaka 2025.   












































Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com