Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAKUBEL AVUTA FOMU KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA TANGA

Na Hadija Bagasha Tanga

Joto la uchaguzi limezidi kupanda katika jiji la Tanga baada ya Mwalimu Kassim Amar Makubel  kujitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kuomba ridhaa CCM kugombea Nafasi ya Ubunge Jimbo la Tanga. 

Makubel amechukua fomu kwa katibu wa CCM wilaya ya Tanga Jamal Khimji mapema leo asubuhi katika ofisi za chama hicho jiji la Tanga. 

Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuchukuwa fomu hiyo Makubel amesema kuwa uongozi wa Rais Samia umemvutia kuweza kuona ipo haja kugombea ili kuunga mkono juhudi hizo .

"Nia yangu ni kuomba ridhaa kwa wanaccm kuweza kuwatumika wanatanga hivyo nawaomba waniunge mkono katika dhamira hii ya kuwaletea maendeleo wananchi wenzangu "amesema Amar.

"Nimejitokeza leo kuchukua fomu ili kuwania kuteuliwa na kupata ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi katika jimbo letu la Tanga ili kuweza kupeperusha bendera ya chama chetu katika uchaguzi huu mwezi Oktoba, "amesema Makubel.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com