
Msanii mkongwe wa Hip Hop Tanzania, Professor Jay, ameachia wimbo mpya unaoitwa “Ebenezer” akishirikiana na staa wa muziki kutoka Uganda, Jose Chameleone, na mwanamuziki mahiri Q Chief (sasa akijulikana kama Q Chilla).
Wimbo huu ni wa kumshukuru Mungu kwa ulinzi na neema katika maisha, huku kila msanii akitoa ujumbe wa kipekee unaogusa maisha ya kila siku. Professor Jay ameimba kuhusu maovu yanayoikumba dunia, wakati Chameleone ametumia Kiswahili na Kiingereza kuonesha shukrani zake kwa Mungu. Q Chief ameupamba wimbo kwa sauti yake tamu ya uimbaji wa kiroho.
“Ebenezer” ni ushirikiano wao wa kwanza baada ya miaka 17, na tayari umepokelewa kwa kishindo kwenye mitandao ya kijamii na YouTube.
🔗 Tazama video hapa: Ebenezer - Professor Jay x Chameleone ft. Q Chief
Social Plugin