Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAANDISHI WA HABARI WATUA SHINYANGA GIRLS SECONDARY SCHOOL! MSIGWA 'SERIKALI INAENDELEA KUIBORESHA'

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema kuwa Serikali itaendelea kuiboresha Shule ya Sekondari ya Wasichana Shinyanga (Shinyanga Girls Secondary School) ili kuifanya kuwa shule bora zaidi nchini.

Bwana Msigwa ametoa kauli hiyo leo wakati wa ziara yake mikoa ya Mwanza na Shinyanga, akiwa pamoja na waandishi wa habari kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Ameeleza kuwa Shule ya Wasichana Shinyanga ni miongoni mwa miradi mikubwa ya kielimu iliyotekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 4, na tayari ujenzi unaendelea ili kuhakikisha mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia kwa wanafunzi wa kike.

“Shule ya Wasichana Shinyanga ni mradi wa kimkakati katika kuwekeza kwa wasichana kielimu. Serikali itaendelea kuboresha mazingira haya ili kuifanya shule hii kuwa miongoni mwa shule bora kabisa nchini,” amesema Msigwa.

Shule ya Sekondari ya Wasichana Shinyanga ni mojawapo ya shule 26 maalum za wasichana nchini, ambapo ilianza rasmi kupokea wanafunzi mwaka 2023 kwa ngazi ya kidato cha kwanza na cha pili, pamoja na kuwa na wanafunzi wa kidato cha tano na sita kwa mchepuo wa Sayansi.

Picha na Kadama Malunde

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com