Wanawake wa mkoa wa Simiyu wakiendelea na shamra shamra za maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Imeelezwa kuwa mkoa wa Simiyu unaendelea kupinga kwa nguvu zote jamii ambayo haizingatii usawa wa kijinsia katika nafasi mbalimbali za uongozi mkoani humo ambapo wanajamii wa mkoa huo, wametakiwa kuwekeza katika kuwawezesha wanawake na wasichana katika nyanja mbalimbali kwani ujenzi wa taifa lolote duniani hauwezekani pasipokuwa na ushirikiano wa wanawake na wanaume.
Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Simiyu Kenani Kihongosi wakati akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani humo ambayo yamefanyika leo Machi 03, 2025 wilayni Busega, ambapo amesisistiza ushirikishwaji wa wanawake katika nyanja mbalimbali.
“Nitoe wito kwa jamii nzima ya mkoa wa Simiyu, tuendelee kusomesha watoto wa kike, na kuhakikisha ushirikishwaji wa wanawake katika maamuzi na uongozi, bila ubaguzi katika ngazi zote, ili kukamilisha ulingo wa Beijing inatakiwa utetezi wa haki za wanawake na wasichana uwekwe katika vitendo kwa kutenga bajeti zinazozingatia usawa wa kijinsia, wanawake kushirikishwa kwenye maamuzi, nafasi za uongozi na katika kumiliki mali”. Amesema Kihongosi
Akizungumza katika maadhimisho hayo mkuu wa wilaya ya Bariadi Simon Simalenga, akawaasa wanawake kutobaki nyuma na badala yake wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
“Baadhi ya maeneo iliaminika kwamba mwanamke sehemu yake ya kukaa ni jikoni, sasa hivi mambo yamebadilika, nchi inaongozwa na mwanamke jemedari chifu Hangaya Dkt. Samia Suluhu Hassan na nchi imetulia kweli kweli, kwahiyo niwaombe sana mwaka huu kwenye uchaguzi kinamama mjitokeze kwa wingi kwenda kugombea kwenye kata, majimbo na viti maalum.” Amesema Simalenga.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Busega Faidha Salim, akaeleza kuwa wilaya hiyo inaendelea kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri inayotolewa kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Mkuu wa wilaya ya Bariadi Simon Simalenga, akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wanawake yaliyofanyika leo mkoani Simiyu katika wilaya ya Busega, na kuwaasa wanawake kuchangamkia fursa za uongozi katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Mkuu wa wilaya ya Busega akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika leo mkoani Simiyu katika wilaya ya Busega, ambaye ameeleza kuwa serikali wilayani humo inaendelea kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri, ambayo hutolewa Kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu.
.
Wanawake mbalimbali wa mkoa wa Simiyu wakiwa katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika leo wilayani Busega mkoani humo.
Social Plugin