Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

GST YAONGEZA MAKUSANYO YA NDANI KUTOKA WASTANI WA BIL. 1.25 HADI BIL. 2.39



Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Katika kipindi cha miaka minne cha Serikali ya Awamu ya Sita, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imeongeza makusanyo ya ndani kutoka wastani wa shilingi bilioni 1.25 mwaka 2021 hadi bilioni 2.39 mwaka 2023/2024, sawa na ongezeko la asilimia 91.32.

Pia, idadi ya sampuli zinazochunguzwa imeongezeka kutoka wastani wa 19,184 mwaka 2021 hadi 25,793 mwaka 2023/2024, ongezeko la asilimia 34.45. Bajeti ya taasisi iliongezeka kutoka bilioni 10 mwaka 2021/2022 hadi bilioni 110 mwaka 2024/2025, ongezeko la asilimia 1,000, likilenga kukamilisha majukumu mbalimbali ya taasisi, ikiwemo miradi ya maendeleo.

Hayo yameelezwa leo March 27,2025 Jijini Dodoma na Mkurugezi wa Huduma za maabara GST Notka Banteze kwenye mkutano wake na Waandishi wa habari ambapo ameeleza GST pia ilikamilisha utafiti wa jiolojia katika maeneo ya QDS 278 na 290, yaliyopo Hifadhi ya Taifa ya Mwalimu Nyerere na Pori la Akiba la Selous, katika mikoa ya Lindi na Ruvuma.

"Matokeo ya awali yanaonesha uwepo wa rasilimali mbalimbali za madini, ikiwemo mchanga wa ujenzi, madini ya dhahabu, urani, kaolin, chokaa, udongo mfinyanzi, silica sand, madini tembo, na metali adimu,utafiti wa madini ya viwandani ulifanyika, ambapo jumla ya madini viwandani 44 yalibainishwa, miongoni mwao yakiwemo madini muhimu kama vile kinywe, "amesema.

Aidha,ameeleza kuwa utafiti wa madini ya helium ulifanyika katika mikoa ya Arusha, Manyara, Dodoma, Singida, na Shinyanga, ambapo kiwango cha helium kilibainika kwenye chemchem za majimoto zinazofaa kwa hatua ya utafiti wa kina katika maeneo ya Ziwa Natron, Ziwa Eyasi-Arusha, Maswa, na Ngaka.

"Katika mwaka wa fedha 2024/2025, GST ilikamilisha utafiti wa jiolojia katika maeneo ya QDS 278 na 290, yaliyopo Hifadhi ya Taifa ya Mwalimu Nyerere na Pori la Akiba la Selous, katika mikoa ya Lindi na Ruvuma,Matokeo ya awali yanaonesha uwepo wa rasilimali mbalimbali za madini, ikiwemo mchanga wa ujenzi, madini ya dhahabu, urani, kaolin, chokaa, udongo mfinyanzi, silica sand, madini tembo, na metali adimu, "ameeleza

Licha ya hayo amesema utafiti wa madini ya viwandani ulifanyika, ambapo jumla ya madini viwandani 44 yalibainishwa, miongoni mwao yakiwemo madini muhimu kama vile kinywe huku utafiti wa madini ya helium ulifanyika katika mikoa ya Arusha, Manyara, Dodoma, Singida, na Shinyanga, ambapo kiwango cha helium kilibainika kwenye chemchem za majimoto zinazofaa kwa hatua ya utafiti wa kina katika maeneo ya Ziwa Natron, Ziwa Eyasi-Arusha, Maswa, na Ngaka.

Amesema katika mwaka wa fedha 2024/2025, GST ilikamilisha utafiti wa jiolojia katika maeneo ya QDS 278 na 290, yaliyopo Hifadhi ya Taifa ya Mwalimu Nyerere na Pori la Akiba la Selous, katika mikoa ya Lindi na Ruvuma.

"Matokeo ya awali yanaonesha uwepo wa rasilimali mbalimbali za madini, ikiwemo mchanga wa ujenzi, madini ya dhahabu, urani, kaolin, chokaa, udongo mfinyanzi, silica sand, madini tembo, na metali adimu. Pia, utafiti wa madini ya viwandani ulifanyika, ambapo jumla ya madini viwandani 44 yalibainishwa, miongoni mwao yakiwemo madini muhimu kama vile kinywe,

Utafiti wa madini ya helium ulifanyika katika mikoa ya Arusha, Manyara, Dodoma, Singida, na Shinyanga, ambapo kiwango cha helium kilibainika kwenye chemchem za majimoto zinazofaa kwa hatua ya utafiti wa kina katika maeneo ya Ziwa Natron, Ziwa Eyasi-Arusha, Maswa, na Ngaka, "amesema.

Kwa upande wa ushirikiano wa kimataifa, GST imeendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali za kimataifa katika utafiti na usimamizi wa rasilimali madini. Hii ni pamoja na kushirikiana na taasisi za kigeni katika tafiti za jiolojia na mafunzo ya wataalamu, ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.

Amesema katika mwelekeo wa mwaka 2025/2026, GST itaendelea kuimarisha tafiti za jiolojia na utafiti wa madini, ikiwa ni pamoja na kuongeza maeneo ya utafiti na kuboresha huduma za maabara na kwamba itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika sekta ya madini, ili kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali madini kwa maendeleo ya taifa.






Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com