Mkutano wa tatu wa nchi zinazolima zao la Kahawa Afrika wenye kauli mbiu ya kufungua fursa za ajira kwa vijana kupitia uhuishaji wa Sekta ya Kahawa Afrika.
Mjadala umejikita juu ya ni kwa namna gani nchi za Afrika zinatakiwa kufanya ili sekta hiyo itoe ajira kwa vijana na kuongeza maendeleo ya kiuchumi Afrika.
Akiwasilisha hotuba yake katika mkutano huo Waziri wa Kilimo Tanzania Mhe Hussen Bashe amesema "Wakati Afrika inazalisha asilimia 50 ya Kahawa yote duniani lakini Kahawa inayo nywewa Afrika inaagizwa toka nje ya bara la Afrika na sababu kubwa ñikuwa Afrika inauza nje Kahawa ghafi badala ya Kahawa iliyosindikwa"
Aidha amezitaka nchi za Afrika kuungana badala ya kushindana kwani ilivyo kwa kwa sasa ni rahisi kuuza Kahawa nje ya Afrika na ni ngumu kuuzia nchi jirani yako Kahawa amesema.
Amesema ni vyema nchi za Afrika zikaungana katika sekta ya kahawa kwani mageuzi ya uzalishaji katika sekta hii hayaletwi na mtu mmoja mmoja.
Social Plugin