SILLO AKUTANA NA KAMATI YA KUDHIBITI, KURATIBU MAPATO YA SERIKALI





Na Dotto Kwilasa, DODOMA

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Daniel Sillo aongoza Kikao cha Kamati ya Kusimamia, Kudhibiti na Kuratibu Mapato na Matumizi ya Serikali ya Wizara hiyo kwa Robo ya Nne ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 jijini Dodoma Leo Septemba 19, 2024

Naibu Waziri Sillo akizungumza katika kikao hicho alipitia taarifa ya Kamati ya Kusimamia, Kudhibiti na Kuratibu Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Robo ya Nne ya Mwaka wa Fedha 2023/2024.

Sambamba na kupokea taarifa za mapato na matumizi kutoka kwenye Idara zote na Vyombo vya Usalama vilivyo chini ya Wizara hiyo, ikiwemo Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Uhamiaji pamoja na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)

Kikao hicho kimehudhuriwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Seperatus Fela, Wakuu wa Idara na Viongozi mbalimbali wa Vyombo vya Usalama vilivyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post