WABUNGE WAKOSHWA NA TBA KATIKA MAONESHO YA SEKTA YA UJENZI




Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana,akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Meneja Usimamizi Miliki TBA,Fredy Mangula,wakati alipotembelea Banda la TBA katika Maonesho ya Sekta ya Ujenzi kuelekea Bajeti ya Wizara hiyo yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma ambayo yanashirikisha Taasisi zote zilizoko chini ya Wizara ya Ujenzi.

Na Alex Sonna-DODOMA

WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) imeonesha kazi inazofanya kwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Maonesho ya Sekta ya Ujenzi huku Wabunge wakiipongeza kwa kuitekeleza kwa wakati na kiwango.

Akizungumza leo Mei 28,2024 katika viwanja wa Bunge jijini Dodoma katikae maonesho ya Sekta ya Ujenzi kuelekea Bajeti ya Wizara hiyo yalifanyika Kaimu Meneja Mawasiliano na Masomo (TBA) Fredrick Kalinga amesema lengo la maonesho hayo ni kuonesha mafanikio ambayo wameyapata katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema katika utekelezaji wa miradi hiyo TBA kuna maeneo wapo kama washauri elekezi na wasimamizi.

Amesema kuna maeneo wanatekeleza miradi kama wakandarasi ambapo mshauri anaweza kuwa kampuni nyingine.

Amesema kuna sehemu wanatekeleza miradi kama washauri elekezi na kama wakandarasi

"TBA wanajukumu la kutoa makazi kwa viongozi wa Umma ambapo kwa Mkoa wa Dodoma wameweza kujenga katika eneo la Kisasa na wanaendelea na mradi wa nyumba 3600 katika eneo la Nzuguni ambapo nyumba za awamu ya kwanza 150 zimekamilika na zingine 150 zinaendelea."amesema Bw.Kalinga

Pia amesema wameenda kuwaonesha wabunge kuhusiana na utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan kuitaka TBA kutekeleza sheria ambayo ilianzishwa ili kushirikiana na sekta binafsi.

Amesema katika kutekeleza huko lengo ni kuhakikisha kwamba miradi ambayo inatekelezwa wanaongeza spidi na kuongeza idadi ya fedha.

"Tupo hapa kuonesha miradi ambayo tumejipanga nayo kutekeleza kwa njia ya ubia kati yetu na sekta binafsi,"amesema Kalinga.

Ameitaja moja ya mradi huo ni ule ambao unapatikana Dar es salaam katika eneo la Magomeni Kota ambapo kwa Dodoma ni eneo la Nzuguni,Mwanza ni Ghana Kota na utekelezaji wa ujenzi wa maghorofa mawili kati ya sita tayari umeanza.

"Tunatarajia maghorofa hayo yakikamilika yataenda kuchukua watu wengi zaidi.Tupo katika maeneo mbalimbali ila tumeanza na Majiji kwa kushirikina na sekta binafsi.

"Sambamba na hayo tumekuwa tukiwaonesha wabunge 'clip' mbalimbali za umuhimu wa wabunge kulipa Kodi ambazo zinatusaidia kufanya ukarabati,"amesema Kalinga.

Pia amesema wamewaonesha wabunge jinsi wanavyoshirikiana katika miradi ya kimkakati kama Mji wa Serikali ambapo wanahusika katika majengo 19 kama mshauri elekezi na jengo moja la Utumishi ambapo limeishakamilika kama mkmdarasi.

Kuhusu ulipaji wa madeni,Bw.Kalinga amesema : " Hali ya ulipaji imekuwa nzuri na hivi tunavyozungumza zoezi linaendelea katika Mkoa wa Mwanza,"

Amesema zoezi hilo litakuwa endelevu katika Mikoa mingine Tanzania Bara.

Kwa upande wake Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanislaus Mabula ameipongeza TBA kwa tekeleza miradi kwa kiwango cha Kimataifa.

"TBA imekuwa kielelezo cha ufanyaji kazi katika Nchi hii miradi yao inaubora katika hili naomba niwapongeze,"amesema Mhe. Mabula.

Aidha Mhe.Mabula amesema licha ya Ubora wa miradi hiyo lakini TBA wanatakiwa kujenga miradi katika maeneo yote nchini.


Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana,akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Meneja Usimamizi Miliki TBA,Fredy Mangula,wakati alipotembelea Banda la TBA katika Maonesho ya Sekta ya Ujenzi kuelekea Bajeti ya Wizara hiyo yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma ambayo yanashirikisha Taasisi zote zilizoko chini ya Wizara ya Ujenzi.


Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya,akiwa katika Banda la TBA katika Maonesho ya Sekta ya Ujenzi kuelekea Bajeti ya Wizara hiyo yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma ambayo yanashirikisha Taasisi zote zilizoko chini ya Wizara ya Ujenzi.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Bw Ludovick Nduhiye,akisalimiana na watumishi wa TBA kwenye Banda la TBA katika Maonesho ya Sekta ya Ujenzi kuelekea Bajeti ya Wizara hiyo yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma ambayo yanashirikisha Taasisi zote zilizoko chini ya Wizara ya Ujenzi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post