RC FATMA MWASSA KUMJENGEA NYUMBA BI. CATHERINE ATHANAEL ATHARI ZA MAFURIKO


Nyumba ya Bi Catherine Atanael
Mkuu wa mkoa wa Kagera Fatma Mwassa akizungumza na Wananchi walioathiriwa na mafuriko

Na Mariam Kagenda - Kagera

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajath Fatma Mwassa amemuahidi kumpatia kiwanja na kumjengea nyumba bi. Catherine Athanael miaka 60 ambaye  nyumba yake imedondoshwa na mafuriko katika mtaa wa Migera manispaa ya Bukoba na huku akiwa na jukumu la kuwalea  wajukuu zake sita ambao ametelekezewa na watoto wake.


Mwassa ametoa kauli hiyo wakati akikagua nyumba ambazo zimeathirika na mafuriko ya mvua katika manispaa ya Bukoba.

Amesema kuwa ofisi yake imeguswa na maisha anayoishi  mjane huyo na hivyo amehaidi kumpatia kiwanja na kumjengea nyumba ya vyumba viwili ili aweze kupata mahali pa kujiifadhi na  ametumia nafasi hiyo kuwataka watoto wa bibi huyo kurudi nyumbani ili waweze kulea watoto wao na kuwa serikali iko tayari kuwapatia mitaji ili wafanye biashara na kuweza kuwatunza watoto wao.

Kwa upande wake bi. Catherine Athanael amesema kwa sasa hana pa kuishi na amehifadhiwa na msamaria mwema pamoja na hao wajukuu wake na hajui hatima ya maisha yake kwani afya yake inazidi kuzorota na kufafanua kuwa  kati ya wajukuu hao sita ni yatima kwani  wazazi wao walishafariki.
Bi Catherine akiwa na wajukuu zake

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post