BEI YA ZAO LA PAMBA 2024/2025 YATANGAZWA RASMI, WAKULIMA WATAKIWA KUENDANA NA SOKO LA KIMATAIFA


Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Wizara ya kilimo kupitia bodi ya pamba nchini imetangaza bei elekezi ya ununuzi wa zao la pamba katika msimu wa mwaka 2024/2025 ambayo ni Sh 1,150/=  kwa kilo 1 ya pamba.

Sherehe hizo zilizoambatana na uzinduzi wa ununuzi wa zao la  pamba kitaifa 2024/2025  zimefanyika leo katika Kijiji cha Ndoleleji Wilaya ya Kishapu Mkoa wa Shinyanga, ambapo wanunuzi wote wa pamba watatakiwa kununua kwa bei elekezi iliyotangazwa na serikali katika msimu huu.

 

Akitoa bei hiyo Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Dafroza Ndalichako amesema wilaya ya Kishapu ni kati ya Wilaya zinazofanya vizuri katika uzalishaji wa zao la pamba lakini bado kuna changamoto ya kuwa na pamba chafu na kutokukata masalia ya pamba ambayo yanashusha uzalishaji na kupunguza dhamani ya zao hilo.

“Msimu huu wa mwaka 2024/2025 bei elekezi ya serikali ya kununua pamba ni Sh 1,150/=  kwa kilo moja na makampuni yote yanayonunua yanatakiwa kununua kwa bei hiyo na siyo chini ya bei iliyotangazwa”, amesema Ndalichako. 

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya pamba Tanzania Marco Mtunga amesema wakulima wengi Kishapu bado  wanalima kilimo cha mazoea kwa kusia na kumwaga mbegu za pamba badala ya kupanda kwa kufuata kanuni za kilimo.

Mtunga amewataka wakulima kuzingatia ubora wa pamba wanayozalisha ili kuwa na kilimo chenye tija ikiwa ni pamoja na kuepuka kuweka maji, mchanga na kuhakikisha wanavuna katika utaratibu mzuri ili kuepuka kuweka uchafu jambo linalosababisha kushuka kwa dhamani ya zao hilo katika soko la nje.

Kwa uande wake balozi wa zao la pamba nchini Bwana Agrey Mwanri amemshukuru mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani pamoja na waziri wa kilimo Mheshimiwa Hussein Mohamed Bashe kwa kutoa bilioni 1.8 kwa halmashauri ya kishapu kutokana na jitihada zilizofanywa na wananchi huku akisisitiza matumizi bora ya pembejeo sambamba na kuzingatia namna bora ya utunzaji wa zao hilo hata baada ya kuvuna.

Zoezi la kukata utepe kuashilia uzinduzi rasmi wa bei ya zao la pamba. 

<<<<<<TAZAMA PICHA>>>>>

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Dafroza Ndalichako akikabidhi fedha kwa mkulima wa zao la pamba aliyeuza mazao yake.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu William Jijimya akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Kishapu , Shija Ntelezu akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani akizungumza wakati wa sherehe hizo za uzinduzi.
Mbunge wa Jimbo la Kishau Boniphace Butondo akizungumza wakati wa sherehe hizo za uzinduzi.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa NEC, Gasper Kileo akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza wakati wa uzinduzi huo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post