TCRA KUWATAMBUA WATOA HUDUMA ZA UTANGAZAJI ,MAUDHUI MTANDAONI WANAOFANYA VIZURI

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania  (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari akizungumza wakati wa warsha hiyo

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Dkt Jabiri Bakari amewasisitiza waandishi wa habari na watoa huduma za utangazaji kuzingatia maadili,kanuni na sheria za kutoa huduma hiyo kwani  sekta hiyo ina mchango mkubwa    katika kujenga jamii bora na kuleta maendeleo ya jamii na Taifa.

Dkt. Bakari amesema hayo leo Jumatano Mei 29,2024 katika warsha kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Mwanza iliyoandaliwa na TCRA ili kuwajengea uwezo na kuwakumbusha kanuni za utangazaji na maudhui mtandaoni.

Dkt. Bakari  amesema lengo la TCRA ni kukuza ubunifu na kuwapa nafasi ya kuanzia vijana wasio na ajira rasmi hivyo watumie fursa ya mtandao katika kujenga jamii bora.

Aidha Dkt. Bakari amesema TCRA imeshaanza mchakato wa kuwatambua  watoa huduma za utangazaji, blogs na maudhui mtandaoni wanaofanya vizuri katika kufuata kanuni na ubunifu 

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Jabiri Bakari.

“Sisi tunaozalisha na kusambaza taarifa zinazoenda kwa watu walio wengi, wapokeaji taarifa wanatengenezwa kutegemeana na taarifa ambayo wameipokea,” amesema Dkt Bakari.

Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum amesema Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inahimiza ushindani katika utoaji wa huduma bora ili kuchangia ustawi wa wananchi na maendeleo.

"TCRA itaendelea kushirikisha wadau katika kutatua changamoto katika ukuaji wa sekta ya utangazaji lakini pia tutaendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha sekta ya Utangazaji inatoa mchango katika maendeleo ya nchi",amesema Mhandisi Imelda.

Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda.

"Endapo namba ya simu, email unayotumia kuwasiliana na TCRA haipo, tafadhali weka taarifa ili iwe rahisi kwa mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuwasiliana na watoa huduma, sisi hatuhitaji kumuacha mtu nyuma, tunataka kila mmoja wetu atumie mfumo wetu wa Tanzanite Portal. Tunataka tufanye mawasiliano kupitia mfumo huu".

"Uhalisia ni kwamba Teknolojia imebadilisha mambo mengi, hivyo Vyombo vya habari vinatakiwa kuwa wabunifu ili vipate Matangazo. Vipindi vyenye viashiria vya kuhamasisha Ushoga haviruhusiwi, tusiiachie mamlaka, ukiona kuna kipindi chenye viashiria vya ushoga kwenye chombo cha habari, toa taarifa TCRA", ameongeza Mhandisi Imelda.

Kwa upande wao waandishi wa Habari wameishukuru Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwa warsha za mara kwa mara za kukumbushana kanuni za utangazaji
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania  (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari akizungumza katika warsha ya Watoa huduma za maudhui katika vyombo vya habari Mkoa wa Mwanza iliyoandaliwa na TCRA leo Jumatano Mei 29,2024
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania  (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari akizungumza katika warsha ya Watoa huduma za maudhui katika vyombo vya habari Mkoa wa Mwanza
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania  (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari akizungumza katika warsha ya Watoa huduma za maudhui katika vyombo vya habari Mkoa wa Mwanza

Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum akizungumza katika warsha ya Watoa huduma za maudhui katika vyombo vya habari Mkoa wa Mwanza

Afisa Mawasiliano TCRA Judith Nyange akizungumza katika warsha hiyo
Afisa Mawasiliano TCRA Judith Nyange akizungumza katika warsha hiyo
Afisa Mawasiliano TCRA Judith Nyange akizungumza katika warsha hiyo
Afisa Mawasiliano TCRA Alpha Wawa akizungumza katika warsha hiyo
Afisa Mawasiliano TCRA Alpha Wawa akizungumza katika warsha hiyo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post