WANANCHI FUATILIENI TARATIBU NA MAELEKEZO YA SERIKALI KUKABILIANA NA MADHARA YATOKANAYO NA MVUA-DKT. YONAZI


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi akizungumza na waandishi wa Habari amabao hawapo katika picha, katika eneo maarufu kwa jina la Daraja la Masai, lililopo katika barabara ya uhuru Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza mara baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua maeneo yaliyoathiriwa na mvua zinazoendelea.

Aliyesimama Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Baladya Eliakama, akizungumza kuhusiana na madhara ya mvua zinaoendelea kunyesha katika mkoa wa Mwanza kabla ya kuanza kwa ziara ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu ya kutembelea maeneo yaliyoathiriwa na Mvua hizo.

Kati picha (katikati) Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge n Uratibu Dkt. Jim Yonazi na wataalam kutoka Ofisi ya Mkoa wa Mwanza, TARURA, TANROADS na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu wakiwa katika ziara ya kutembelea baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa na Mvua zinazoendela kunyesha, Mkoani Mwanza

Wataalam kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu wakiwa katika kikao kabla kuanza kwa ziara ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge n Uratibu Dkt. Jim Yonazi ya kutembelea baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa na Mvua zinazoendela kunyesha mkoani Mwanza.

Katika ni sehemu ya kingo za miundombinu ya Daraja unapopita mto Nyamilongo Wilayani Nyamagana lilivyoharibiwa na mvua zinazoendela kunyesha Mkoani Mwanza.




NA. MWANDISHI WETU – MWANZA


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amewataka wananchi kuzingatia na kufuata taratibu zinazotolewa na Serikali ili kuweza kukabiliana na madhara yatokananyo na mvua hasa za El nino kuweza kuokoa maisha na mali zao.

Ameyasema hayo Januari 20, 2024, Jijini Mwanza alipokuwa katika ziara ya kukagua hali ya Mafuriko katika Jiji la Mwanza ambapo mvua la El nino zinazoendelea zimeleta athari mbalimbali na kuharibu miundombinu pamoja na mali za watu.

Dkt. Yonazi amesema ni muhimu sana wananchi kuwa wazalendo na kufuata maelekezo ya serikali kwa sababu suala zima la uokoaji ni gharama.

“Suala hili ni gharama kwa Serikali lakini pia inaweza kugharimu maisha hivyo ni muhimu sana pale ambapo tumeelekezwa na Serikali kufuata taratibu tuweze kufuata taratibu.” Alisisitiza.

Katibu Mkuu Dkt. Yonazi amebainisha kuwa kwa wananchi ambao wameelekezwa kuhama katika maeneo hatarishi waweze kuhama ili waweze kulinda maisha yao, mali zao na maisha ya jamii kwa ujumla na ametoa wito kwa wananchi kote nchini kufuata taratibu, miongozo na maelekezo halali ya Serikali na ndiyo namna ya kujilinda dhidi ya mafuriko na majanga.

Amewataka pia wananchi kushiriki katika miradi mikubwa akitolea mfano mradi wa ujenzi wa kingo za mto Nyamilongo unaopita katika wilaya ya Nyamagana ili maji yake yasiende katika makazi ya watu na kuharibu mali nyingine na kufahamu kwamba ushiriki wao utaleta faida katika maana ya kutunza mali zao, mali za asili na kuhakikisha kwamba maisha yanaendelea vizuri.

Katika hatua nyingine,Dkt. Yonazi amewaasa watumishi wa umma kufuata utaratibu hasa katika kusimamia suala zima la ujenzi holela, kwani unapofanyika ujenzi holela ni rahisi sana kupata madhara.

“Ili kuweza kuwa na makazi bora kwa wananchi wetu ni vizuri kuhakikisha maisha hayahatarishwi na mafuriko na hata yanapotokea mafuriko inakuwa rahisi kuokoa.” Amesema Dkt. Yonazi

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Elikana amesema, mvua hizi za El nino kwa baadhi ya maeneo katika mkoa wa Mwanza zimeleta uharibifu wa baadhi ya miundombinu kama vile madaraja na Barabara.

Aidha amepongeza Wakala wa Barabara vijijini na Mijini (TARURA) mkoani Mwanza kwa kuendelea kufanya kazi kubwa ya kuhakikisha kwamba miundombinu hiyo inarejea katika hali yake ya kawaida.

Sambamba na hilo aliongelea suala la mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu mkoani humo, ambapo alisema ulianzia katika Wilaya ya Magu na kufika katika wilaya ya Ilemela na Nyamagana ambapo Serikali ya mkoa kwa kiasi kikubwa imechukua hatua, tahadhari pamoja na Kudhibiti.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post