BENJAMIN MKAPA FOUNDATION NA NMB ZAUNGANA KULETA MAGEUZI

 

NMB Foundation na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation imesaini rasmi makubaliano ya ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili, ikiwa na lengo la kutekeleza miradi ya pamoja kwenye eneo la kijamii (afya na elimu).

 Ushirikiano huo yamesainiwa Jana January 25 katika ukumbi wa mikutano wa benki ya NMB, na yanategemewa kuwa makubaliano ya muda wa miaka mitatu.

Maeneo makuu ya kimkakati ya NMB Foundation ni kwenye  Afua au Sekta ya Elimu, Afya, Kilimo, Mazingira na Ujasiriamali.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utiaji Saini,Meneja Mkuu wa Taasisi ya NMB Nelson karumuna amesema, lengo kuu la NMB Foundation ni kukuza ujumuishaji endelevu na mpana wa kiuchumi kupitia mchanganyiko wa ufadhili, uvumbuzi wa kijamii, na utaalam wa kiufundi, ili kuharakisha matokeo. 

Amesema tangu kuanzishwa kwake mwaka 2021, NMB Foundation imetekeleza miradi mbalimbali katika sekta ya elimu na kilimo, na sasa inaingia rasmi katika eneo la afya na Elimu kwani hizi ni sekta zinazoshabihinia ama kutegemeana.

 "Makubaliano haya na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation yanakuja katika kipindi ambapo nchi yetu inaendelea kupiga hatua kubwa kufikia malengo ya SDG ifikapo 2030 na Dira ya Maendeleo ya Kitiafya ya mwaka 2025."alisema Karumuna

Amesema ni dhahiri kwamba ushirikiano huu walioingia  kati yao utakua na tija katika kuongeza nguvu kwenye Program zinazotekelezwa na Serikali Tanzania bara na Zanzibar.  

"Kama taasisi inayotekeleza miradi ya kijamii, NMB Foundation inategemea makubwa sana kutokana na mashirikiano haya na huu ni ushirikiano kati ya taasisi mbili zenye ushawishi katika maeneo yake ya kiutendaji na Sisi tupo zaidi katika sekta ya kifedha na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation ni nguli katika eneo hili la afya na elimu, hivyo ni mategemeo yetu kuwa kuunganishwa kwa nguvu zetu kwa Pamoja kutawezesha miradi mingi kuanzishwa na kuwafikia watanzania wengi zaidi Tanzania Bara na Zanzibar.

" Tumejiwekea lengo la kukusanya kwa pamoja rasilimali fedha kutoka kwa vyanzo mbalimbali wakiwemo wadau wa maendeleo/wafadhili, wasamaria wema na sekta binafsi ikiwemo pia NMB Bank.” Alisema  Karumuna.

Kwa upande wake Ofisa Mtedanji Mkuu Taasisi ya Benjamin Mkapa Dk Ellen Senkoro  amesema taasisi hiyo imekua kinara wa utekelezaji wa miradi ya afya nchini, kuanzia ngazi ya Taifa hadi kwenye jamii kwa Tanzania Bara na Zanzibar. 

"Kwa miaka 18 sasa, Mkapa Foundation imekuwa ikitekeleza afua za kuimarisha mifumo ya sekta ya afya ndani ya hospitali/vituo vya tiba na kwenye jamii inayopelekea kuboresha Afya ya Uzazi, na kupambana na maradhi ya kuambukizwa na kutoambukiwa yakiwemo ya milipuko.,"

"Baadhi ya afua ambazo Taasisi ya Mkapa imebobea ni kwenye kubuni na kutoa ajira za watumishi wa afya zaidi ya 11,000, kuimarisha miundo mbinu ya Vituo vya tiba na hospitali na kushirikisha jamii na asasi za kiraia kwenye utoaji wa huduma za afya na pia kushiriki katika uandaaji na utekelekezaji wa sera na miongozo ya sekta ya Afya.," alisema   Dkt Ellen

Amesema NMB Bank na NMB Foundation ni mfano dhahiri ambapo imetambua kwamba kwa kushirikiana na Taasisi ya BMF yenye uzoefu na ujuzi kwenye program za afya na elimu, basi tutawafikia watanzania kwa uharaka zaidi na kupata matokeo makubwa.

 " Tunatambua kwamba Sekta ya afya imekua ikizalisha kiasi kikubwa cha wataalamu kwa mwaka (takribani 10,000) na baadhi yao hupata ajira katika utumushi wa umma au sekta binafsi ikiwemo kujiari wenyewe na haya mashirikiano yatalenga kuwasaidia wataalam hawa wa afya waongezewe elimu, stadi na ujuzi, na pia fursa za ajira ndani na nje ya nchi”. Alisema Dkt. Ellen.

NMB Foundation na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation zinaamini katika mashirikiano kama chachu ya kuleta maendeleo endelevu katika jamii. Makubaliano haya ni mwanzo wa utekelezaji wa miradi yenye lengo la kuendel


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments