KATAMBI AGAWA MAJIKO YA GESI YA ORYX KWA MABALOZI WA CCM, WENYEVITI WA VITONGOJI KUTUNZA MAZINGIRA

 

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,amegawa majiko ya Gesi kwa Mabalozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, huku akimpongeza Rais Samia kwa kuleta Maendeleo jimboni humo.
Zoezi la Ugawaji wa Majiko hayo ya Gesi limefanyika leo Januari 26,2024 katika ukumbi wa Mikutano wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga.

Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, akizungumza wakati wa kugawa majiko hayo, amesema anawathamini sana viongozi hao, ndiyo maana ameamua kuwapatia majiko ya gesi nishati ambayo ni safi na salama kupikia pamoja na kutunza Mazingira.
"Mabalozi wa CCM mnafanya kazi kubwa ya kukitumikia Chama na Serikali, hivyo Mimi nina wathamini sana na kuwaheshimu ndiyo maana tumekutana hapa leo tufurahi, tujadili namna ya kuendelea kuimarisha Chama, na kuwapatia majiko ya gesi," amesema Katambi.

Aidha, amempongeza Rais Samia kwa kumpa ushirikiano na kusukuma Maendeleo katika Jimbo la Shinyanga, na miradi mingi imetekelezwa na kuubadilisha mji huo huku bado akiendelea kutoa Mabilioni ya fedha ikiwamo kujenga Stendi kubwa ya Mabasi na Kisasa.
"Nyie wenyewe mnaona Maendeleo makubwa katika Mji huu wa Shinyanga ndani ya miaka yangu Minne ya Ubunge ahadi nyingi nimezitekeleza na nina Mshukuru Rais Samia amenisaidia sana, Shinyanga ya sasa siyo kama yazamani imepiga hatua kubwa kimaendeleo," ameongeza Katambi.

Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anorld Makombe, amempongeza Mbunge huyo kwa kuwathamini Mabalozi wa CCM na kuwapatia majiko hayo ya Gesi pamoja na kula nao chakula.
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Ally Majeshi, amempongeza Mbunge Katambi kwa kufanya kazi za Serikali, kuwatumikia wananchi,pamoja na kazi za Chama na wana CCM wamefurahi, huku akikemea suala la Majungu kwa viongozi.

Mkuu wa Kitengo cha Mauzo Tanzania Bara kutoka ORYX Gesi Alex Wambi, amesema matumizi ya Gesi ni Nishati Mbadala ya kutumia katika kutunza Mazingira na kudhibiti ukataji wa miti hivyo kwa ajili ya kuni za kupikia.
Nao baadhi ya Mabalozi hao, wameshukuru Mbunge huyo kwa kuwathamini, na kubainisha kwamba hakuna Mbunge ambaye amewahi kuwajali Katambi ndiyo wa kwanza.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu akizungumza kwenye hafla na Mabalozi wa CCM ya kuwakabidhi Majiko ya Gesi.
Katambi akiendelea kuzungumza na Mabalozi wa CCM.
Katambi akiendelea na kuzungumza na Mabalozi wa CCM.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Anorld Makombe akizungumza kwenye hafla hiyo.
Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Ally Majeshi akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Mauzo Tanzania Bara kutoka ORYX Gesi Alex Wambi akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mabalozi wa CCM wakiwa kwenye hafla hiyo.
Hafla ikiendelea ya kukabidhiwa Majiko ya Gesi.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea ya kukabidhiwa Majiko ya Gesi.
Hafla ikiendelea ya kukabidhiwa Majiko ya Gesi.
Hafla ikiendelea ya kukabidhiwa Majiko ya Gesi.
Hafla ikiendelea ya kukabidhiwa Majiko ya Gesi.
Hafla ikiendelea ya kukabidhiwa Majiko ya Gesi.
Hafla ikiendelea ya kukabidhiwa Majiko ya Gesi.
Elimu ya Matumizi ya Gesi ikitolewa kwa Mabalozi hao.
Elimu ya Matumizi ya Gesi ikiendelea kutolewa.
Katambi (katikati) akiwa na Mwenyeketi wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Anorld Makombe (kulia) wakipokea Majiko ya Gesi kutoka ORYX kwa ajili ya kuwapatia Mabalozi wa CCM.
Zoezi la ugawaji Majiko ya Gesi kwa Mabalozi wa CCM likiendelea.
Zoezi la ugawaji Majiko ya Gesi kwa Mabalozi wa CCM likiendelea.
Zoezi la ugawaji Majiko ya Gesi kwa Mabalozi wa CCM likiendelea.
Zoezi la ugawaji Majiko ya Gesi kwa Mabalozi wa CCM likiendelea.
Zoezi la ugawaji Majiko ya Gesi kwa Mabalozi wa CCM likiendelea.
Wafanyakazi kutoka ORYX wakipiga picha ya pamoja.

CHANZO - SHINYANGA PRESS CLUB BLOG


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post