WARSHA YA ASASI ZA KIRAIA YAJA NA MATUMAINI KWA JAMII ILIYOSAHAULIKA


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Katika kilele cha Warsha ya Asasi za kiraia,iliyokuwa ikiendeshwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)Wametoa mapendekezo yao katika dira ya Taifa ya 2050 kutokana na changamoto walizozibaini katika dira ya Taifa ya 2025 katika Mambo yenye mlengo wa kijinsia.

Hayo yamesemwa leo Desemba 22,2023 Jijini Dar es Salaam na Afisa Programu na Sera kutoka Idara ya Ujenzi wa harakati nguvu za pamoja (TGNP) Bi.Logathe Loakaki alipokuwa akizungumza katika kilele cha warsha ya Asasi za kiraia ambayo imehusisha washiriki kutoka Kanda mbalimbali nchini.

Amesema kuwa wameangazia mambo mbalimbali katika dira ya Taifa 2025,katika nyanja tano ambazo ni Utamaduni,Siasa, uchumi,Jamii kwa lengo la kutambua dira imefanikiwa kiasi gani na changamoto zilizopo katika mlengo wa kijinsia.

"Kwahiyo tumeangazia dira katika hayo maeneo,kwa kiasi gani dira imeweza kujibu masuala au mahitaji yale makundi ya pembezoni na kutokana na mambo yaliyo ibuliwa wali weza kutengeneza mapendekezo tunapo elekea dira ya 2050 dira iweje, mambo gani yazingatiwe ili kuhakikisha usawa na maendeleo endelevu ya nchi kwa ujumla"Bi.Logathe Amesema.

Aidha Bi.Logathe amesema kuwa wadau kutoka Asasi za kiraia wameridhia na kuahidi kuhusu mapendekezo waliyo toa na mambo waliyo ibua kutoka katika dira hiyo yatakua chachu ya kuielimisha Jamii ili waweze kujihusisha katika Mchakato wa dira Taifa ijayo.

"Walipofika jana kwenye Warsha tulipo anza kujadiri mambo ya dira ya Taifa wengi walionesha kwamba hawakuwa wameifahamu vya kutosha na wengine hawakuwahi kuifahamu kwahiyo imekuwa fursa ya kujua dira hii kwa kutambua ombwe hilo basi katika Jamii pia hawaifahamu dira hiyo"Amesema

Pamoja na hayo ametoa wito kwa Jamii ya watanzania waishio ndani ya nchi na nje ya nchi kushiriki katika kutoa mapendekezo yao katika dira mpya ya 2050 ili kujihusisha na Mchakato huo wa dira ya Taifa kwa kutoa maoni yao kwa kubonyeza namba *152*00#kisha namba 8 Elimu,alafu kubofya 4 dira.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Vijana ya Right for Success,Bi.Zena Mulokozi Amesema kuwa katika Mambo ya usawa wa kijinsia Kuna mambo yako sawa na mengine hayako sawa ambapo katika dira mpya ijayo inatakiwa kuzingatiwa ili kumpa ahueni mwanamke.

"Ukija mfano sahivi kwenye kuna suala la changamoto ya nauli zimependa anaye hangaika sana ni mwanamke mwenye hali ya chini kwasababu anafanya biashara yake kwa kutumia usafiri wa umma Sasa gharama ikipanda mia moja kwake no maumivu makubwa sana ikipanda mia mbili kwake ni maumivu makubwa sana, ukiangalia hakuna mwanaume anabeba beseni kwenda kuuza mboga,serikali katika dira mpya iangalie hata kwenye suala la nauli ikiwezekana zitofautiane Kati ya mwanaume na mwanamke"Bi Zena Ameeleza.

Naye Meneja wa Programu kutoka Shirika la Builders of Future Africa,Bw.Frank Sakalani ameeleza kuwa Asasi za kiraia wamejadiri mambo ambayo haya kuwepo katika mpango wa maendeleo endelevu wa dira ya Taifa 2025 na kuyatambua ili kuyaweka katika dira mpya ya 2050 ili ioneshe wazi katika mambo ya masuala ya kijinsia.

TGNP imepanga kuichambua dira na kuweka mapendekezo yake pamoja na kuambatanisha mapendekezo ya Asasi za kiraia na kuwasilisha kwa serikali ambapo wanatarajia kuanzisha kampeni kwa kutumia vyombo vya habari kuhamasisha umma kuhusu dira hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post