RC MNDEME AWASHA UMEME KWENYE KIJIJI KILICHOKOSA UMEME TANGU NCHI IPATE UHURU... ATOA MAELEKEZO KWA MKANDARASI


Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amewasha umeme kwenye kijiji cha Kahanga kata ya Wandele Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama.

Zoezi hilo la uzinduzi limefanyika leo Desemba 13, 2023, katika kijiji cha Kahanga ikiwa ni hitimisho la ziara ya kutembelea miradi inayotekelezwa wilayani Kahama.

Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Mkandarasi kutoka Shirika la usambazaji umeme Tanzania TANESCO Antony Tarimo amesema  utekelezaji wa mradi huo wa usambazaji wa umeme katika manispaa ya Kahama Mpaka sasa mkandarasi amefanikiwa kuwasha vijiji 16 kati ya vijiji 29 na vijiji 10 kazi zinaendelea.

"Kijiji hiki ni miongoni mwa vijiji 29 ambavyo vitanufaika na mradi huu pale itakapokamilika. Mradi unatekelezwa na mkandarasi TONTAN PROJECT TECHNOLOGY LTD ambaye alianza utekelezaji wa mradi huu tarehe 14 Feb 2022 na kutarajiwa kumalizika ifikapo tarehe 31 Desemba 2023 ukihusisha ujenzi wa miundombinu ya msongo wa kati wenye urefu wa Kilomita 54.99, urefu wa msongo mdogo Kilometa 28.69 ufungaji wa transifoma 29 pamoja na shughuli nyingine", amesema Antony Tarimo.


"Mpaka sasa mkandarasi amefanikiwa kuwasha umeme kwenye vijiji 16 kati ya vijiji 29 vijiji 10 kazi zinaendelea ambapo katika kijiji hiki cha Kahanga mkandarasi amejenga laini ya msongo wa kati yenye kilometa 5.8 miundombinu imekwisha kamilika na siku ya leo tumezindua kwenye kaya hii pamoja na wateja wengine ambao wameshaunganishiwa mita, zoezi la uhamasishaji linaendelea tukiwa na imani wananchi wengi watajitokeza kuunganishiwa", ameongeza Mhandisi Antony Tarimo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kahama Thomas Mnyonga ameipongeza serikali kupitia Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kufikisha umeme kwenye kila kijiji hapa nchini.


"Tuendelee kumuunga mkono Rais wetu aendelee kuleta fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi ndani ya wilaya ya Kahama, wote ni mashahidi tunashuhudia ilani ya Chama cha Mapinduzi ikiendelea kutekelezwa kikamilifu kwenye sekta mbalimbali, niwatoe hofu wakazi wa Kahama ", amesema Thomas Mnyonga.

Mkuu wa mkoa Shinyanga Christina Mndeme amewahakikishia uhakika wa upatikanaji wa umeme mara baada ya kumalizika kwa mradi wa usambazaji umeme ifikapo Dwsemba 31, 2023 huku akimsihi mkandarasi kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huo.


"Hongereni sana kwa kupata umeme, Serikali imetenga Shilingi Bilioni 363 kwa ajili ya miundombinu ya umeme nchini, leo hii historia imeandikwa mara baada ya kuwasha umeme kwenye kijiji hiki tangu nchi imepata uhuru, mkandarasi huyo amepatiwa shilingi bilioni 32 kwa ajili ya kusambaza umeme kwenye vijiji 146 ndani ya wilaya ya Kahama ambapo shilingi bilioni 5.5 zitatumika kusambaza umeme kwenye Manispaa ya Kahama mkiwemo ninyi wakazi wa kijiji cha Kahanga", amesema RC Mndeme.

"Maelekezo yangu kwa mkandarasi vijiji vyote ambavyo havijafikiwa hakikisha ifikapo tarehe 31 Desemba, 2023 vijiji vyote viwe vimefikiwa na huduma ya umeme, wananchi hawa hawataki kuona waya na nguzo wanataka kuona taa zikiwaka majumbani kwao hivyo ongezeni kasi ya utekelezaji", ameongeza RC Mndeme.

Ukaguzi wa miradi ukiendelea ndani ya wilaya ya Kahama.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kulia) akiteta jambo na mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita.

Wananchi waliojitokeza kwenye hafla ya uzinduzi wa kuwasha umeme kwenye kijiji cha Kahanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akikata utepe kwenye uzinduzi huo.
Kikundi cha Sungusungu kata ya Wandele kikitumbuiza wakati wa hafla hiyo.Katibu tawala mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post