TARURA MNAFANYA KAZI NZURI: WAZIRI BASHUNGWANa Mwandishi Wetu,Arusha

Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa ameipongeza Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA ) kwa kazi nzuri wanazofanya na za utekelezaji wa  majukumu yake ya kuzifungua barabara nchini.

“TARURA mnaupiga mwingi kwenye Ujenzi wa madaraja na barabara za mawe,mfikishieni salamu zangu Waziri wa OR-TAMISEMI,Mtendaji Mkuu pamoja na watumishi wote wa TARURA.

Mhe. Bashungwa ameyasema hayo leo tarehe 30 Novemba, 2023 alipotembelea banda la maonesho la TARURA kwenye Kongamano la Kitaifa la 32 la Taasisi ya Wahandisi Tanzania linalofanyika Kituo cha Kimataifa cha Mkutano cha Julius Nyerere Arusha (AICC).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post