WiLDAF YAFANYA MAFUNZO YA USAWA WA KIJINSIA KWA RAFIKI SDO


Na Deogratius Temba, Shinyanga

Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WILDAF),imefanya mafunzo ya kujenga uwezo kwa wafanyakazi  na Menejimenti ya Shirika la RAFIKI SDO la Shinyanga, namna ya kuingiza masuala ya Kijinsia katika Programu na muundo wa shirika kwa ujumla. 

Mafunzo haya ni sehemu ya mradi unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (Sida) kupitia Save the Children-Tanzania, kwa lengo la kukuza uwezo wa asasi  za kiraia, kuimarisha mifumo ya kitaasisi na kuongeza sauti za watoto kujadili, kujisimamia  na kudai haki zao za msingi,unaotekelezwa kwa ushirikiano  na WILDAF, RAFIKI SDO na wadau wengine watano. 

Akizungumza katika mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa RAFIKI SDO, Tangi Clement, mafunzo hayo yamewafungua macho kujiangalia Zaidi kwa undani jinsi wanavyotekeleza masuala ya Kijinsia kama taasisi lakini pia namna ambavyo program na miradi ya shirika inavyolenga kutatua changamoto za kijinsia katika jamii hasa wanufaika wa miradi. 

“Tunaishukuru sana WILDAF kwa kutupatia mtaalamu wa Jinsia kutupatia elimu hii, bado sisi kama RAFIKI SDO tunajifunza kwenye eneo la Jinsia, ni fursa muhimu sana ambayo tumeipata, tutahakikisha tunayafanyia kazi kikami,ifu ikiwepo kupeleka elimu hii kwa wafanyakazi ambao hawakushiriki, lakini pia wadau wetu kama Halmashauri za wilaya tutawapa elimu hii sambamba na wanufaika wetu”, alisema Tangi. 

Ameongeza kwamba katika warsha hiyo, wamekubaliana kwamba kunahitajika mapitio ya sera za ndani kama mapitio ya mwongozo wa rasilimali watu ili kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyakazi wenye ujauzito kupata muda wa kupumzika na iwepo sehemu maalum kwaajili hiyo.
 
Aidha wamependekeza kwamba, mapitio ya sera ya Jinsia yaende sambamba na kuingiza suala la Usawa na Haki kijinsia kwa watu wenye ulemavu na Mama aneyenyonyesha akiwa ndani shughuli za shirika kuhudumiwa yeye na mtoto wake kikamilifu. 

“Hii itahitaji mabadiliko ya kisera, kuwasilisha kwa manajimenti na bodi ili kupata Baraka zao, lakini ni jambo nzuri tuna Imani watatusikiliza”,aliongeza.

Pia, waliweka mkakati wa kuweka uzito katika uchechemuzi kwenye Halmashauri za wilaya ili kutenga bajeti yenye mrengo wa Kijinsia aitakayowezesha watoto wa kike kusoma na kuwa salama ndani nan je ya shule kama kupata mlo wa chakula cha mchana shuleni ili kupunguza utoro na mimba za utotoni, kujenga mabweni na kuwezesha wasichana wa shule za sekondari kupatia taulo za kike. 

Naye mwezeshaji kutoka WiLDAF, Deogratius Temba, amesema kwamba, WiLDAF inamatumaini kwamba, baada ya mafunzo hayo, mabadiliko makubwa ya kitaasisi yatatokea kwani washiriki wameweka ahadi (commitiment) ya kuweka nguvu kwenye mabadiliko ya kitaasisi ili  kila kitu kinachofanyika ndani ya shirika kiweze kuwa na mtazamo wa Kijinsia.

Ameongeza kwamba, mafunzo haya yamepelekea washiriki kukubaliana kupitia upya sera ya jinsia ya Rafiki SDO ya mwaka 2022, na Mpango Mkakati wake wa (2020-2024) ili kuweza kuzingatia usawa wa Kijinsia na kuweka bajeti ya ndani ya Taasisi itakayotatua changamoto wa Kijinsia. 

“Sisi tuna Imani, kama walivyosema washiriki hawa wa RAFIKI SDO, Baada yam waka mmoja tukirudi hapa kutakuwa na mabadiliko makubwa” ,amesema Temba. 

Kwa upande wake Programu Meneja wa Rafiki SDO Mkoa wa Geita, Eliud Mtalemwa alisema kwamba mafunzo haya yameisaidia taasisi kujiona vizuri Zaidi, kutambua namna inavyosimamia masuala ya Kijinsia na mapengo yalipo kwani  inahitaji kuweka miongozo ya Kijinsia itakayowasimamia. 

 “Tumeona kwamba, wanawake wanashiriki kwenye shughuli zetu na kwenye nafasi za maamuzi lakini hatuna kitu kinachotuongoza na kutulazimisha kwa namba, kwamba wanawake wawe wangapi kwenye hizo nafasi, kwa elimu tuliyopipata hapa,tumefunguka, tutaboresha kwa kupitia upya nyenzo zetu za kiutendaji", alisema Mtalemwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post