WATUMISHI TAMISEMI WATEMBELEA KITUO CHA FARAJA - IRINGANa Asila Twaha, Iringa

 Watumishi wa Ofisi ya Rais, TAMISEMI wanaoshiriki Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) kwa kushirikiana na uongozi wa Shirikisho hilo wametembelea na kutoa misaada yenye thamani ya sh 900,000 kwenye kituo kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Faraja kilichopo Halmashuri ya Manispaa ya Iringa.

Akizungumza kwa niaba ya watumishi wa TAMISEMI Sports Club Oktoba 13, 2023 Yunis Shimwela amesema wameona ni vyema kuwatembelea watoto na kutoa misaada ikiwa ni sehemu ya furaha yao ya kushiriki SHIMIWI.

Naye, Mjumbe wa SHIMIWI, Yustina Bubinza amesema lengo lao ni kuonesha  upendo,furaha na umoja kwa watoto hao huku akimshukuru Rais Mhe. Dkt.Samia Suluh Hassan kwa kuruhusu kuendelea kuwepo kwa michezo hiyo na watumishi.

Kwa upande wake, Mlezi wa Kituo cha Faraja  Franco Sordella amewashukuru kwa misaada hiyo ambayo itasaidia watoto 72 wanaolelewa wenye umri kuanzia miaka tatu na kuendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post