VIKUNDI 45 VYA SANAA KUSHIRIKI TAMASHA LA BAGAMOYO FESTIVAL 2023

Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamomoyo (TaSUBa) Dkt. Herbert Makoye akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 25,2023 Bagamoyo mkoani Pwani kuhusu kuelekea uzinduzi wa Tamasha la 42 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ambalo linatarajiwa kuzinduliwa Oktoba 26,2023 na mgeni Rasmi Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro.

****************

NA EMMANUEL MBATILO, PWANI

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Tamsha la 42 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (Bagamoyo Festival) ambalo litafanyika Oktoba 26,2023 kwenye Viwanja vya TaSUBa Bagamoyo mkoani Pwani.


Akizungumza na Waandishi wa habari leo Oktoba 25,2023, Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamomoyo (TaSUBa) Dkt. Herbert Makoye amesema katika tamasha hilo, vikundi 45 vya sanaa ambapo 34 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar huku vingine vikitoka nchi mbalimbali vitashiriki kuonesha umahili wao katika sanaa.

Amesema lengo la tamasha hilo ni kuvutia wadau wa sanaa kutoka ndani na nje ya nchi ikiwemo kutangaza utamaduni na vivutio mbalimbali ambavyo vinapatikana kwenye maeneo tofauti tofauti.

"Tamasha la mwaka huu kutakuwa maonyesho ya wajasiriamali ambayo yatahusisha taasisi 15 za serikali na sanaa za ufundi zitashirikisha washiriki 30 na pia washiriki watapata fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo Wilaya ya Bagamoyo vikiwemo Mji Mkongwe, Kaole na Boma la Wajerumani". Amesema Dkt. Makoye.

Pamoja na hayo Dkt. Makoye amesema kuwa nchi zilizothibitisha kushiriki tamasha la hilo msimu huu wa 42, ni pamoja na nchi ya Canada, Botswana, Afrika Kusini, Uganda, Zambia, Burundi na Kenya.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post