TBS YAWATAKA WADAU KUSHIRIKI KWENYE UANDAAJI WA VIWANGO


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Katika kuadhimisha Siku ya Viwango Duniani, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limewataka wadau na wananchi kushiriki vyema katika uandaaji wa viwango ili kwa pamoja tuweze kuandaa viwango vinavyotekelezeka .

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Oktoba 13,2023 Jijini Dar es Salaam, Meneja wa Viwango Bw.Yona Afrika amesema kuna umuhimu mkubwa wa wadau kushiriki katika uandaaji wa viwango kwani viwango vinasaidia uzalishaji wa bidhaa bora nchini na kuweza masoko makubwa ndani na nje ya nchi.

Aidha amesema kuwa viwango vinasaidia kupunguza gharama pamoja na kukuongezea wateja kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi.

Amesema suala la uandaaji wa viwango linahusisha wadau wote wa uzalishaji wa bidhaa na sio la Shirika la Viwango pekee.

Siku ya Viwango Duniani huadhimishwa kila ifikapo Oktoba 14 kila mwaka

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post