MASHINDANO YA UVCCM SHY TOWN DR. SAMIA CUP YAHITIMISHWA KWA KISHINDO...TIMU YA UVCCM NDEMBEZI YAONDOKA NA MILIONI 5, KOMBE

Na mwandishi wetu Malunde 1 Blog Shinyanga

Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Mhe. Lucy Mayenga amehitimisha rasmi ligi maalum ya DR. SAMIA CUP SHINYANGA MJINI iliyolenga kuinua vipaji kwa vijana wanaocheza mchezo wa mpira wa miguu katika Wilaya ya Shinyanga mjini.

Fainali hiyo imehitimishwa leo Jumamosi Oktoba 21,2023 katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM) mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi CCM wakiwemo wabunge pamoja na madiwani katika Manispaa ya Shinyanga na nje ya Manispaa.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Mhe. Lucy Mayenga ameipongeza taasisi ya Bega kwa Bega na Mama kwa ubunifu huo, kushirikiana na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Shinyanga mjini katika kuandaa mashindano ya mpira ambayo yametoa fursa mbalimbali kwa vijana walioshiriki ligi hiyo.

Mhe. Mayenga akiwa kwenye hafla ya kuhitimisha ligi ya DR. SAMIA CUP SHINYANGA amekabidhi kiasi cha shilingi milioni tatu kwa timu iliyoshika nafasi ya pili ambayo ni Timu ya Rangers kutoka Tanroads pamoja zawadi nyingine kwa msindi wa kwanza na mshindi wa tatu.

 Pia Mhe.Mayenga amekabidhi zawadi zilizotolewa kwa mshindi wa mashindano hayo ambapo mshindi wa kwanza ambaye ni timu ya UVCCM Ndembezi amekabidhiwa kombe pamoja na fedha shilingi milioni tano ,Mshindi wa pili Rangers kutoka Tanroads amekabidhiwa shilingi milioni tatu  na Mshindi wa tatu ambaye ni UVCCM Ngokolo amekabidhiwa Shilingi milioni 2.

Naye Mratibu wa Mashindano ya Dr. Samia Cup Shinyanga Mjini, Jackline Isaro amesema lengo la mashindano hayo ni kukuza vipaji na kutengeneza ajira kwa vijana wilayani humo pamoja na kuchochea maendeleo ya mchezo wa soka.

Isaro amesema katika mashindano hayo ambayo yamefikia tamati leo timu 3 ambazo ni UVCCM Ndembezi ,Rangers kutoka Tanroads na UVCCM Ngokolo zimeibuka kidedea kati ya timu 32 ambazo zimeshiriki mashindano hayo.

“Sisi kama taasisi ya Bega kwa Bega na Mama Samia tunaunga mkono juhudi za Mhe. Rais Samia kwa kuhamasisha michezo na sasa tumehitimisha mashindano ya mpira wa miguu ambayo yameshirikisha timu 32 na kufanyika kwa muda wa mwezi mmoja na nusu kuanzia Agosti 27,2023 katika viwanja vinane Shinyanga Mjini",ameeleza Isaro.

"Mashindano haya tumeyaita Samia Viwanjani kwa kuwa tunaona Mhe. Rais wetu Dr. Samia Suluhu Hassan anapenda michezo hivyo taasisi ya Bega kwa Bega kwa kushirikiana na Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini tumefanya mashindano haya ambayo yatakuwa mashindano endelevu kwa kumuunga mkono Rais wetu kwa kupenda michezo hususani mpira wa miguu. ",ameeleza.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Ushetu Mhe.Emanwel Cherehani ameipongeza kamati ya maandalizi hayo kwa kufanikisha mashindano hayo ambayo yametoa fursa kwa vijana wa Manispaa ya Shinmyanga.

 Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akikabidhi shilingi milioni 5 kwa timu ya UVCCM Ndembezi

Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akikabidhi shilingi milioni 5 kwa timu ya UVCCM Ndembezi

Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akikabidhi kombe kwa timu ya UVCCM Ndembezi


































Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post