MNH-MLOGANZILA YAFANIKIWA KUFANYA UPASUAJI WA KUPUNGUZA UZITO KWA WAGONJWA WANNE

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 31,2023 katika hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila Jijini Dar es Salaam.

**********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili Mloganzila imefanikiwa kufanya upasuaji wa kibingwa bobezi wa kupunguza uzito kwa wagonjwa wanne wenye uzito uliokithiri ambapo zoezi hilo ni mara ya kwanza nchini katika Hospitali za Umma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 31,2023 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi amesema utaratibu huo wa matibabu umefanyika kwa njia ya utaalamu wa hali ya juu bila upasuaji ambapo wagonjwa watatu wamefanyiwa kwa njia ya matundu madogo (Laparoscopic Sleeve Gastrectomy) na mmoja amefanyiwa kwa kutumia njia ya Endoskopia (Endoscopic Sleeve Gastroplasty).

Amesema kwa kutumia endoskopia mtu atapoteza uzito kwa asilimia 15-23, na kwa kutumia matundu madogo (Laparoscopic Sleeve Gastrectomy) atapoteza uzito kwa asilimia 50-70 ndani ya miezi kumi na mbili.

“Utaratibu huu wa matibabu kwa watu wenye uzito uliopitiliza umefanywa na Madaktari Bingwa Bobezi wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (Upanga&Mloganzila) kwa kushirikiana na mtaalamu bobezi wa upasuaji kutoka nchini India Dkt. Mohit Bhandari pamoja na Taasisi ya Medincredi”. Amesema

Aidha amesema kuwa kila mmoja amefanyiwa huduma hii kwa muda wa takribani dakika 15 mpaka 30 ambapo watatu waliruhusiwa baada ya masaa 24 baada ya kupatiwa huduma na mwingine aliruhusiwa saa nane baada ya huduma.

“Kwa upande waliofanyiwa huduma hii wa juu kabisa alikuwa na uzito Kilogramu 142 na wa chini alikuwa na uzito wa Kilogram 107, ambapo tunategemea baada ya kupata huduma hii watapungua uzito wao kwa kiasi kikubwa”. Ameeleza Prof.Janabi

Prof.Janabi amesema lengo ni kuhakikisha huduma hizo zinakuwa endelevu ambapo mpango wa hospitali ni kuwezesha huduma hizo kufanyika kila mwezi na kwa siku za usoni zitakuwa zinafanywa na wataalamu wa ndani.

Ameeleza kuwa wanatoa pia huduma mbalimbali za Kibingwa Bobezi ikiwemo kupandikiza figo, kupunguza uzito kwa kutumia puto maalum (intra gastric balloon), kuondoa uvimbe kwenye sakafu ya ubongo kwa matundu ya pua, kuvunja mawe kwenye figo kwa kutumia mawimbi mtetemo, kupandikiza nyonga bandia na upasuaji wa kutumia matundu madogo.
Prof.Janabi amempongeza Rais Dkt, Samia Suluhu kwa kuwekeza katika sekta ya afya ambapo amenunua vifaa tiba kuanzia ngazi ya Zahanati hadi kwenye hospitali bobezi ya Taifa na kuweza kumpunguzia gharama mgonjwa kutafuta tiba nje ya mipaka ya nchi.

"Wote mnaelewa changamoto ya fedha za kigeni, hawa tusingewafanyia upasuaji hapa wangetafuta njia moja au nyingine kwenda nje maana yake wangetumia fedha za kigeni"Amesema
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 31,2023 katika hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 31,2023 katika hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 31,2023 katika hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 31,2023 katika hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 31,2023 katika hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 31,2023 katika hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Madaktari wabobezi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi  wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 31,2023 katika hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post