KATAMBI AWAPOKEA UVCCM TAIFA NA KUWAPONGEZA KUELEKEA KILELE CHA MWENGE WA UHURU MANYARA



Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amewapongeza vijana wa UVCCM Taifa kwa kujitambua na kuwa wazalendo katika kulijenga Taifa lao.  

Amesema maendeleo ya Taifa lolote yanahitaji vijana wanaojitambua, wanaofahamu historia ya nchi yao, wanaojali Afya zao, wakatambua wajibu wao, wakafanya kazi kwa bidii na wakawa msitari wa mbele katika kuunga mkono jitihada zinazo fanywa na serikali.

Mhe. Katambi amebainisha hayo Oktoba 12, 2023 wakati akiendelea na ukaguzi wa uwanja wa Kwaraa Mkoani Manyara ambapo yatafanyika maadhimisho ya kilele cha Mwenge wa uhuru kitaifa 2023

Aidha, amesema Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imeandaa mazingira wezeshi na fursa za ajira kwa vijana  ili kutimiza malengo waliyojiwekea  ikiwa ni pamoja kutoa programu za kukuza ujuzi, mikopo kwa mtu mmoja mmoja ili wajikwamue kiuchumi.

Hata hivyo, Mhe. Katambi  amekagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa Kwaraa na kuridhishwa nao kwa pamoja wananchi wa Manyara wapo tayari kumpokea Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge kitaifa 2023..

Chama Cha Mapinduzi ni mlezi wa vijana na tunajivunia kuwa na chama makini hakika vijana wa chama cha mapinduzi ni hazina ya taifa "amesema Katambi".


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post