TANZANIA, AUSTRIA KUSHIRIKIANA KATIKA AJIRA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Waziri Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu   imekubaliana kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Austria juu ya kufungua fursa za ajira  kwa watanzania nchini humo.

Ajira hizo zitawahusisha watanzania wenye ujuzi na ambao hawana na kuwaongezea ujuzi katika sekta ya kilimo, viwanda  na biashara. 

Makubaliano hayo yamefikiwa leo katika Mkutano wa Naibu Waziri Ofisi hiyo Mhe. Patrobas Katambi  na Waziri wa Kazi na Uchumi Austria Prof. Martin Kocher  Oktoba 25, 2023 Jijini Dar es salaam.

Mhe. Katambi amesema wamekubaliana kujifunza namna ambavyo wanaendesha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na  elimu ya ufundi ambapo hadi sasa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyuo hivyo nchi nzima.

“Austria wana uzoefu, ujuzi na ubobevu katika masuala ya kiuchumi, ajira na elimu hivyo tunataka kutumia nafasi hiyo kufungua fursa kwa vijana wa kitanzania kujifunza namna ambavyo wenzetu wanafanya”  ,amesema


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post