Habari Njemaaa!!! MADAKTARI BINGWA KULETA FURAHA SHINYANGA OKTOBA 27 - 29, 2023...HOSPITALI YA LUCKMED WAMEJIPANGA SANA


 HABARI NJEMA KWA WAKAZI WA MANISPAA YA SHINYANGA NA WANANCHI WOTE KWA UJUMLA. 

Uongozi wa Hospitali ya LUCKMED iliyopo Kizumbi Bugayambele karibu na stendi ya mabasi ya mikoani Ibinzamata maarufu Manyoni na karibu na shule ya Little Treasures katika Manispaa ya Shinyanga, unayo furaha kubwa kuwatangazia wananchi wote kuwa kuanzia tarehe 27/10/2023 hadi 29/10/2023 kutakuwa na ujio wa madaktari bingwa kutoka hospitali ya Rufaa Bugando, hospitali ya rufaa ya Mkoa Shinyanga na hospitali ya Kolandoto watawaona, watawashauri na kuwatibu wagonjwa wa magonjwa mbalimbali ikiwemo na upasuaji

 

 

1. MADAKTARI BINGWA WA UPASUAJI watashughulika na uvimbe uliopo sehemu mbalimbali za mwili pamoja na:



 I. Uvimbe sehemu yoyote kichwani II. Uvimbe shingoni (maarufu kama Goita) III. Uvimbe mdomoni na kwenye koo na Tonsesi IV. Uvimbe tumboni na magonjwa ya kidole tumbo(appendix) V. Uvimbe sehemu za siri na haja kubwa VI. Ngiri za aina zote(Ngiri kavu(Henia) na Ngiri maji(Busha)) VII. Uvimbe mgongoni, mikononi na miguuni. VIII. Uvimbe puani, nyama za puani na kushindwa kupumua IX. Uvimbe kwenye mfuko wa kizazi X. Uvimbe kwenye mfuko wa mayai ya uzazi 

2. DAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA AKINA MAMA NA UZAZI ATAKUWEPO. 

3. DAKTARI BINGWA WA WATOTO ATAKUWEPO

 4. DAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA NDANI ATAKUWEPO Wagonjwa wenye matatizo ya moyo, sukari, figo, vidonda vya tumbo wataonwa. 
5. DAKTARI WA MAZOEZI YA VIUNGO  atakuwepo.

 6. PIA MADAKTARI BINGWA WENGINE WATAKUWA WANATIBU WAGONJWA WAFUATAO; 

I. Wagonjwa walioshindwa kukojoa

 II. Wagonjwa wenye maumivu ya tumbo ya aina yoyote 

III. Wagonjwa walio jisokota utumbo na kushindwa kupata haja kubwa

 IV. Wagonjwa waliovunjika mikono na miguu 

V. Wagonjwa wenye matatizo ya uzazi, macho na miguu. 

VI. Wenye uhitaji wa miwani itakuwepo 

VII .Huduma ya kupima presha na saratani ya matiti zitatolewa bure. 

Namna ya kujiandikisha fika Hospitali ya Luckmed iliyopo Kizumbi Bugayambelele karibu na shule ya Little Treasures. 

Utaandikisha jina lako na tatizo linalokusumbua. Kwa wale ambao mko mbali au ambao hamtaweza kufika tuma ujumbe wasms au piga no 0763-979758/0682-407676/0767-211531/0753- 829014/0762-311531 mwambie ushiriki wako, jina na tatzo linalokusumbua kwa ajili ya kuhudumiwa. 

Na kwa wale watakaokuja siku hiyo ya tukio watapokelewa. 

AFYA YAKO NDIO KIPAUMBELE CHETU; WOTE MNAKARIBISHWA KWA HUDUMA BORA ZA MATIBABU

. ……………………..AHSANTENI……………………. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post