WADAU GDSS WAIPONGEZA SERIKALI KUFANIKISHA UJENZI WA ZAHANATI KILA KATA


WADAU wa semina za Jinsia na maendeleo (GDSS) wamempongeza Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt,Samia Suluhu Hassan,kwa kufanikisha ujenzi wa Zahanati kila kata ambapo imesaidia kupunguza kadhia kwa wanachi kupata huduma kwa wakati na kupunguza vifo.

Pongezi hizo zimetolewa leo Septemba 20,2023 Jijini Dar es Salaam wakati wa Semina za Jinsia na Maendeleo zinazoendeshwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) ambapo mada ambayo walikuwaa wanaizungumzia ni Nyayo zetu fahari yetu ambayo imebeba ujumbe wa mafanikio ya wanaharakati wa jinsia.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mshiriki wa Semina hiyo Bi. Herieth Kabende amesema kuwa kwenye elimu walikua wakiangalia katika masuala waliyokuwa wakiyapigania ambapo ni taulo za kike mashuleni ambazo zitawasaidia watoto wakike kufikia mafanikio.

"Hivi Sasa shule nyingi zipo na zinasaidia kuwepo kwa mahudhirio mazuri kwa mtoto wa kike ingawa baadhi ya shule bado wapo nyuma kwenye suala hili katika kumuwezesha mtoto wa kike asipate changamoto ya kukosa taulo za kike"Amesema.

Aidha Bi. Hariet amesema kwenye suala la Afya ya mama na mtoto walikua wanapigania kupunguza vifo kwa mama na mtoto ambapo amesema hili limefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

"Tumepambana vile vifaa kwa ajili ya kujifungua vipatikane kwenye Zahanati ambapo tulipambana wa mama wapate vifaa hivyo kwenye Zahanati ingawa wapo wamama kijijini wenye uwezo wa kuwa nayo". Amesema

Pamoja na hayo amesema kuwa wameipigania ile sheria ya SOSPA ambayo ilirekebishwa ambayo ilikua imeleta mkanganyiko katika suala la makosa ya kujamiiana ambapo wakati wa nyuma ilikua inamnyima haki mwanamke ambapo alikua anashindwa kufikia fursa anayoitaka.

Amesema kuwa katika suala la Mila na desturi kwenye baadhi ya makabila ambazo zilikua zinamkandamiza mwanamke katika suala la ukeketaji ambapo wanawake walikua wanaona kitu Cha kawaida wanawake wamepata Elimu kupitia hizi semina Mbalimbali za GDSS na serikali hivi Sasa imelivalia njuga kwa kiasi kikubwa.

Hata hivyo amesema kuwa katika suala la uongozi zamani wanawake walikua Kama wapiga debe kwa wanaume nao walishika uongozi lakini Sasa kupitia semina hizi za GDSS wanawake wengi wamepata Elimu na Sasa wengi wameingia katika siasa ambapo wameweza kushika nafasi mbali mbali za uongozi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post