KAMPENI YA UHAMASISHAJI MATUMIZI SAHIHI YA EFD YAZINDULIWA RASMI


MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Ilala imezindua Kampeni ya 'TUWAJIBIKE' ya uhamasishaji juu ya Matumizi sahihi ya EFD.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa kikodi Ilala  Bw! Masau Malima amesema kutoa na kudai risiti  sahihi za EFD  inasaidia kukusanya kodi stahiki kwa maendeleo ya taifa "kodi yetu ndiyo maendeleo yetu" hivyo  amewahimiza wafanyabiashara kutoa risiti kila wanapofanya mauzo na wanunuzi kudai risiti sahihi za EFD kila wanaponunua bidhaa au kupata huduma. Uzinduzi huo umefanyika katika kituo cha huduma za kodi Gongolamboto leo Septemba  08, 2023.

Kwa  upande  wake Mkuu wa kituo cha kodi Gongolamboto Bi. Ambele Mwaisunga amewakaribisha wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kufika katika kituo cha huduma za kodi  Gongolamboto "Tunawakaribisha wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kufika katika kituo chetu cha huduma Gongolamboto". Pia amesema huduma za TRA kwa sasa zimesogezwa karibu na wafanyabiashara katika maeneo yao ya biashara hivyo wasisite kufika na kupata huduma mbalimbali za kodi. 

Aidha wafanyabiashara wameipongeza TRA kwa kusogeza huduma karibu na maeneo yao hivyo kupunguza gharama na muda wa kupata huduma za kodi pia wameishukuru TRA kwa kuendelea kuwakumbusha wafanyabiashara hao wajibu wao juu ya mambo mbalimbali ya kikodi ikiwemo kutoa na kudai risiti.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post