ELIMU YENYE TIJA: AFYA BORA NA USTAWI BORA


Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO, kwa kupitia programu yake ya “Our rights, Our Lives, Our future” inayofahamika kama O3 kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Baraza la maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limefungua mafunzo ya wawezeshaji wa mafunzo ya walimu yanayolenga kutoa elimu ya ufundishaji wa stadi za maisha zinazozingatia afya ya uzazi, VVU/UKIMWI, na kuhusiana kwa heshima.

Mafunzo haya yanatolewa jijini Dodoma kwa washiriki 34 kutoka dayosisi 15 za kanisa katoliki Tanzania kuanzia tarehe 28 Sptemba hadi 06 Oktoba 2023. Ikiwa hii ni awamu ya pili ya mafunzo haya, awamu ya kwanza ilifanyika Julai 2022 ambapo wawezeshaji 54 walipatiwa mafunzo kutoka dayosisi 18 na katika kipindi cha Julai 2022 hadi Agosti 2023 waliweza kufikia walimu zaidi ya 1,300 kwenye shule 355 nchini.

“Wanafunzi hujifunza vyema na kupata matokeo chanya ya elimu yao pale mazingira yao ya kujifunzia yanapokua salama , wao wenyewe kuwa na afya njema na kuwa na uwezo wa kuepuka vikwazo kama vile vya mimba za mapema, magonjwa ya zinaa na UKIMWI na ukatili wa kijinsia ikiwemo unyanyasaji. Mazingira salama ya kjifunza na kufundishia ni ngao ya mafanikio kwa wanafunzi na walimu” – Mathias Luhanya, Msimamizi wa programu ya O3, UNESCO

UNESCO kwa kushirikiana na Serikali kupitia wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Wizara ya afya, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na wadau wa elimu mbalimbali inaunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha mazingira salama ya kujifunzia kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari,ikiwemo kupata elimu sahihi ya makuzi nay a afya ya uzazi inayozingatia umri, mila na desturi, kuzuia ukatili wa kijinsia, elimu ya VVU/UKIMWI na Kuhusiana kwa Heshima.

Mafunzo haya ni sehemu ya mpango wa ushirikiano kati ya UNESCO, Taasisi ya Elimu Tanzania na Kanisa katoliki unaolenga kuboresha mazingira salama ya kujifunza na kufundishia shuleni kupitia kuwajengea uwezo walimu (utoaji mafunzo) na kusambaza miongozo inayohusu utoaji wa elimu husika. Mpango huu unalenga kuwafikia walimu 5000 wa shule za serikali na za taasisi binafsi ifikapo Agosti 2024.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post