DEREVA ALIYESABABISHA AJALI NA KISHA KUKIMBIA ASAKWA


Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamsaka dereva wa basi la Abood lenye namba za Usajili T904 DKY inayofanya safari zake za Dar es salaam na Tabora baada ya kusababisha ajali kwa kuigonga gari aina ya Noah yenye namba za usajili T828 DNB asubuhi ya leo Septemba 11,2023.

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwakwe Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Alex Mkama amesema ajali hiyo imetokea katika eneo la Kitugwa Manispaa ya Morogoro ambapo katika ajali hiyo watu wawili wamepoteza maisha huku majeruhi wawili wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospital ya Mkoa wa Morogoro.

Aidha Kamanda Mkama amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa wa basi la Abood kutumia vibaya barabara jambo lililopelekea kugongana na Noah iliyokuwa ikitokea Morogoro kuelekea Dar es salaam.

Kwa upande wake kaimu afisa Mahusiano wa Hospital ya Mkoa wa Morogoro Scholastic Ndunga amesema kuwa wamepokea Maiti mbili na majeruhi wawili ambao wametokana na ajali hiyo, japo taarifa za awali kutoka kwa Kamanda Mkama zilieleza kuwepo na kifo kimoja na majeruhi watatu.

 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post