DAWASA YAPONGEZWA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UONDOSHAJI MAJITAKA PSSSF


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MBUNGE wa Jimbo la Ubungo Mhe.Kitila Mkumbo amefanya ziara ya kutembelea na kukagua Maendeleo ya Mradi wa Uondoshaji Majitaka wa PSSSF, Sinza - Kijitonyama unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam, (DAWASA).

Akizungumza katika ziara hiyo, Mhe.Mkumbo ameipongeza DAWASA kwa kutekeleza mradi huo kwa ufanisi na amewataka kuongeza nguvu kwa kuweka bajeti ya kutekeleza miradi ili kuondoa adha ya uchafuzi wa Mazingira.

Amesema ni wakati muafaka wa DAWASA kuweka mkakati madhubuti wa kutekeleza miradi ya Majitaka ili kuondokana na uchafuzi wa Mazingira kwenye maeneo korofi ikiwemo Sinza.

"Changamoto iliyopo sasa kwenye maeneo ya Sinza ni uchafuzi wa Mazingira unaosababishwa na utiririshaji hovyo wa majitaka kwenye maeneo ya makazi ya watu". Amesema

Nae Mwakilishi wa Kaimu Afisa Matendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Modesta Mushi ameeleza kuwa utekelezaji wa mradi unalenga kunufaisha kaya zaidi ya 200 za mitaa ya Sinza pamoja na hospitali ya Sinza Palestina.

"Tumejipanga kikamilifu kukamilisha mradi huu mwezi wa kumi, kwa kuwa inatekelezwa usiku na mchana, niwasihi wananchi kuacha kutupa taka ngumu kwenye miundombinu hii kwa kuwa inasababisha kuziba na kuchelewesha ukamilishwaji wa mradi," amesema Mhandisi Modesta.

Ameishukuru PSSSF kwa kutoa ushirikiano wa utekelezaji wa mradi huu unaoleta manufaa ya afya kwa pande zote.

Kwa upande wake Meneja wa Miradi PSSSF Mhandisi Marko Kapinga amesema kuwa mradi huo una manufaa makubwa kuanzia kwa wapangaji wa jengo la PSSSF pamoja na wakazi wanaozunguka jengo hilo na utapunguza kwa kiasi kikubwa magonjwa ya mlipuko.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post