YANGA SC HAIKAMATIKI, YAINYUKA AL - MERRIKH UGENINI, SIMBA SC YALAZIMISHWA SARE

NA EMMANUEL MBATILO
Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania bara wanaendelea kufanya ziara Kimataifa ambapo leo imefanikiwa kuinyuka Al-Merrikh 2-0 mchezo ambao umepigwa kwenye dimba la Pele Kigali nchini Rwanda.

Katika mchezo huo Yanga Sc imeweza kupata mabao kupitia kwa washambuliaji wao Kenned Musonda pamoja na Clement Mzize ambapo mabao yote yamefungwa kipindi cha pili.


Kwa upande wa majirani zao Mabingwa Ngao ya Jamii Tanzania Timu ya Simba SC ambao walikuwa wanakipiga kule Ndola nchini Zambia wamelazimishwa sare ya mabao 2-2, mabao ya Simba Sc yamefungwa na Mzambia Claotos Chama.

 Simba wameshindwa kutamba ugenini katika mechi ya raundi ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika baada ya kulazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya wenyeji Power Dynamos mchezo uliopigwa uwanja wa Levy Mwanawasa nchini Zambia.

Kwa matokeo hayo Simba SC imejiweka nafasi nzuri ya kutinga hatua ya Makundi mchezo wa marudiano utakaopigwa Tanzania Simba inahitaji sare au ushindi wowote.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post