NEMC YATOA MAFUNZO KWA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI GEITA KUEPUKA MADHARA YA ZEBAKI




Mkurugenzi wa Tathmini ya Athari ya Mazingira na Jamii kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC),Bi. Lilian Mkambuz akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, leo Septemba 21 mjini Geita wakati akifungua mafunzo ya uhifadhi wa mazingira katika maonyesho ya matumizi sahihi ya teknolojia ya KAIKA kuinua wachimbaji kiuchumi na hifadhi ya mazingira kwa wachimbaji wadogo mkoani Geita.


Msimamizi wa Mradi wa Kudhibiti matumizi ya Zebaki Tanzania, Dkt.Befrina Igulu, akizungumza leo Septemba 21, 2023 mjini Geita alipokuwa akifungua mafunzo ya uhifadhi wa mazingira katika maonesho ya matumizi sahihi ya teknolojia ya KAIKA kuinua wachimbaji kuchumi na hifadhi ya mazingira kwa wachimbaji wadogo mkoani Geita


Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe.Cornel Magembe akiwa kwenye ufunguzi wa mafunzo ya uhifadhi wa mazingira katika maonesho ya matumizi sahihi ya teknolojia ya KAIKA kuinua wachimbaji kuchumi na hifadhi ya mazingira kwa wachimbaji wadogo mkoani Geita.


Sehemu ya washiriki wakifatilia mafunzo ya uhifadhi wa mazingira katika maonyesho ya matumizi sahihi ya teknolojia ya KAIKA kuinua wachimbaji kiuchumi na hifadhi ya mazingira kwa wachimbaji wadogo mkoani Geita.

Na Mwandishi Wetu, GEITA

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC), limetoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini kuzingatia matumizi sahihi ya zebaki ili kulinda afya zao na kuhifadhi mazingira.

Mkurugenzi wa Tathmini ya Athari ya Mazingira na Jamii kutoka NEMC, Lilian Mkambuz akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, ameyasema hayo leo mjini Geita alipokuwa akifungua mafunzo ya uhifadhi wa mazingira katika maonyesho ya matumizi sahihi ya teknolojia ya KAIKA kuinua wachimbaji kuchumi na hifadhi ya mazingira kwa wachimbaji wadogo mkoani Geita.

Amesema mafunzo hayo yamekuja wakati mwafaka kutokana na ongezeko la wachimbaji linalokwenda sambamba na uharibifu wa mazingira na matumizi ya kemikali za zebaki.

“Hali hii inasababisha athari katika afya ya jamii na uharibifu wa mifumo ya ikolojia iwapo tahadhari hazitachukuliwa katika upangaji na utekelezaji wa matumizi endelevu ya zebaki. Kwa hiyo tunapaswa kuchukua tahadhari kabla ya athari kutokea,”amesema.

Aidha, amesema ili kukidhi matakwa ya Serikali katika kufanikisha azma ya kupunguza uchafuzi utakanao na mtumizi endelevu ya rasilimali za maji, uongo na afya za jamii lengo la kutafiti juu ya teknolojia mbadala zilizoko nchini na zile ambazo zinafanyiwa tafiti mbalimbali na kuzifanyia majaribio na hatimaye zitasambazwa kwa wachimbaji wadogo hapa nchini.

Pia amesema kuwapa elimu juu ya matumizi yake kwa lengo la kuwafanya waondokane na matumizi ya zebaki.

Naye, Msimamizi wa Mradi wa Kudhibiti matumizi ya Zebaki Tanzania, Dk.Befrina Igulu, amesema wameona umuhimu wa kutumia maonesho hayo kutoa elimu kwa wachimbaji hao kujua athari zake matumizi ya zebaki na namna ya kukabiliana nazo.

“Kupitia Mradi huu tutaweza kupitia Sheria na Kanuni zilizopo na kuziboresha kwa kuingiza vipengele vitakavyowezesha usimamizi thabiti wa uingizaji, utunzaji utumiaji na zebaki nchini pamoja na masuala ya utekelezaji,”amesema.

Amebainisha kupitia mradi huo elimu itatolewa kwa wananchi hususan wachimbaji wadogo kuhusu madhara ya zebaki na namna bora ya kuitumia bila kuathiri afya na mazingira.

Naye, Mchimbaji mdogo wa Dhahabu kutoka Geita, Alex Bawaziri, ameishukuru NEMC kwa mafunzo hayo na kuomba serikali iendelee kutafuta kubuni mbinu mbadala kwa ajili ya kudhibiti matumizi ya zebaki.

“Sisi tutaendelea kupunguza matumizi na kuchukua tahadhari katika utumiaji wa zebaki ili usilete madhara katika afya ya binadamu na mazingira,”amesema.

Mchimbaji kutoka Mwanza, Salome Kusekwa, amesema mafunzo hayo yamemsaidia kujua madhara ya zebaki na namna ya kujikinga.

“Tunamshukuru Rais kwa kutuwezesha mafunzo haya kupitia NEMC ,wanawake wachimbaji mimba zilikuwa zikiharibika na kupata shida kwenye uoni wa macho lakini baada ya mafunzo haya tumejua namna ya kutumia zebaki bila ya kuleta madhara kwenye mazingira na afya zetu,”amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post