SERIKALI KUKAMILISHA TAFITI ZA MADINI NCHINI

 

Mpaka sasa utafiti wa kina wa jiofizikia kwa kutumia ndege umefanyika kwa asilimia 16


Serikali kupitia Wizara ya Madini ipo katika mpango wa kukamilisha utafiti wa kina wa  jiofizikia kwa kutumia ndege  kupitia Taasisi ya  Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST).


Hayo yamebainishwa na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde  wakati akihutubia wananchi siku ya ufunguzi rasmi wa maonesho ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita.


Akizungumza juu ya maendeleo ya Sekta ya Madini Mhe.Mavunde alifafanua kuwa Wizara kupitia Dira yake mpya ya 2030 inayosema Madini ni Maisha na Utajiri,  imeona  katika kuchochea ukuaji wa Sekta ya Madini na kuongeza mchango katika Pato la Taifa, kuna haja ya kupata taarifa za miamba na madini kwa eneo lote la nchi yetu.


Alifafanua kuwa katika kutekeleza dira hiyo pamoja na mambo mengine, Serikali itakamilisha utafiti wa kina wa jiofizikia kwa kutumia ndege  kwa asilimia 100 kutoka asilimia 16 zilizopo kwa sasa ifikapo 2030. Lengo la utafiti huo likiwa ni kuchochea zaidi uwekezaji katika Sekta ya Madini pamoja na kufungamanisha sekta ya madini na sekta  nyingine za kiuchumi.


Maonesho ya Sita ya kimataifa ya Teknolojia ya madini yalifunguliwa rasmi Septemba 23 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko na  yatafungwa Septemba  30, 2023.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post