CEO WA MALUNDE 1 BLOG ATEMBELEA OFISI ZA CLEO 24 TV... APONGEZA MATANGAZO LIVE

Mkurugenzi na Kiongozi Mwanzilishi wa Mtandao wa Malunde 1 blog (www.malunde.com)  bw. Kadama Malunde kutoka Mkoa wa Shinyanga ametembelea Ofisi za Runinga ya Mtandaoni (Online Tv) ya Cleo 24 Online Tv zilizopo Tarime Mjini Mkoani Mara.

Malunde ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waandishi wa habari wa Mitandao ya Kijamii (JUMIKITA) Kanda ya Ziwa, amempongeza Mkurugenzi wa Cleo 24 Online Tv, bw. Frankius Cleophace kwa kuanzisha Runinga ya Mtandaoni ambayo mbali na kurusha habari kwa njia za kawaida pia wanarusha habari/matangazo Mubashara (Live) na hivyo kuwa runinga pendwa zaidi katika Kanda ya Ziwa na nchi kwa ujumla.

"Ninampongeza sana kijana Frankius Cleophace kwa kuanzisha Online Tv, ameonesha ubunivu mkubwa hasa kwa kuwekeza nguvu zaidi katika matangazo Mubashara.. Ni kijana anayejituma sana katika kazi. Naamini kabisa chombo hiki kinachomilikiwa na Mwandishi wa Habari kitazingatia maadili ya taaluma ya habari. Uzoefu wangu mtandaoni unaonesha kuwa Vyombo vya habari vinavyoendeshwa na waandishi wa habari vimekuwa vikifanya vizuri sana hasa katika kuondoa changamoto ya Habari za Uzushi na Uongo (Fake News)",amesema Malunde ambaye ni Bloga maarufu Nchini Tanzania.

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Cleo 24 Online Tv, Frankius Cleophace ameahidi kuendesha chombo hicho cha habari kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo mbali huku akisema wamejipanga vyema kuhakikisha wanatoa huduma bora inayokidhi viwango hivyo kuwakaribisha wadau wote katika ofisi zao zilizopo Mjini Tarime.

"Karibuni sana wadau wetu katika Runinga yetu ya Mtandaoni kwa ajili ya huduma za habari, matangazo mbalimbali, karibu katika ofisi zetu , wasiliana nasi kwa simu  namba 0766424928 au 0652583600 ",amesema Frankius

Mkurugenzi na Kiongozi Mwanzilishi wa Mtandao wa Malunde 1 blog, bw. Kadama Malunde kutoka Mkoa wa Shinyanga akiwa katika Ofisi za Runinga ya Mtandaoni (Online Tv) ya Cleo 24 Online Tv zilizopo Tarime Mjini Mkoani Mara.
Mkurugenzi na Kiongozi Mwanzilishi wa Mtandao wa Malunde 1 blog, bw. Kadama Malunde (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi wa Cleo 24 Tv, bw. Frankius Cleophace katika studio za Runinga ya Mtandaoni (Online Tv) ya Cleo 24 Online Tv zilizopo Tarime Mjini Mkoani Mara.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post