MHANDISI MARYPRISCA AFUNGUA MAFUNZO ELEKEZI KWA BODI YA WAKURUGENZI RUWASANaibu Waziri wa Maji, Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Maji , Mheshimiwa Jumaa Hamidu Awesso amefungua mafunzo elekezi kwa bodi ya wakurugenzi RUWASA ambapo yanafanyika Mkoani Iringa.

Wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Mhe. Mahundi amesema kuwa kama Wizara wana amini kuwa maadili ya viongozi ni msingi muhimu wa uongozi bora na wenye tija kwa maendeleo endelevu.

"Hivyo, kwa kusimamia maadili, wajumbe wa bodi mnatakiwa kutekeleza majukumu ya kuiongoza RUWASA. Ni matarajio yangu kwamba mafunzo haya yatawapa mwanga na kuwaimarisha katika kuongoza kwa mfano na kuendeleza maadili ". Amesema

Pia,Mhe.Mahundi amesisitiza kwa Wajumbe wa Bodi kuwa wanahitaji kufahama na kusimamia viashiria hatarishi ili kuhakikisha ustawi na uendelevu wa taasisi. Wajumbe wa Bodi mnahitaji kuwa na ufahamu wa viashiria hatarishi.

Hivyo na kusema kuwa mafunzo haya yatawajengea uwezo wa kutambua, kusimamia, na kupunguza viashiria hatarishi kwa ustawi wa RUWASA.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi RUWASA Bi. Ruth Koya amempongeze Mhe. Rais kwa kumteua kuwa Mwenyekiti wa bodi ya pili ya RUWASA.

Vilevile ameishukuru Wizara ya Maji kwa ushirikiano mzuri wakati wa utekelezaji wa majukumu yake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post