CHADEMA WAFANYA MKUTANO MKUBWA SHINYANGA MJINI, MBOWE , LISSU WAUNGURUMA

 Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Freeman Mbowe, pamoja na Makamu wake Tundu Lissu, wamefanya Mkutano wa hadhara na kuzungumza na Wananchi wa Shinyanga juu ya Mustakabali wa maslahi ya Taifa hasa katika ulinzi wa Rasilimali za nchi na Demokrasia.

Mkutano huo umefanyika leo Agost 25, 2023 katika Viwanja vya Joshoni Lubaga Manispaa ya Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama hicho pamoja na wananchi.

Viongozi hao wakizungumza kwenye Mkutano huo wamegusia suala la Mkataba wa Bandari, Hifadhi, Demokrasia, Katiba Mpya pamoja na kuwapo Tume huru ya Uchaguzi hasa kuelekea kwenye chaguzi zijazo ukiwamo uchaguzi wa Serikali za Mitaa hapo mwakani na Uchaguzi Mkuu 2025.

Aidha, katika Mkutano huo wa hadhara baadhi ya watu walijunga na chama hicho akiwano Thomas ambaye alikuwa diwani wa CCM Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe akizungumza na wananchi wa Shinyanga kwenye Mkutano wa hadhara.
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa Tundu Lissu akizungumza na Wananchi wa Shinyanga kwenye Mkutano wa hadhara.
Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Zanzibar Salum Mwalimu akizungumza na Wananchi wa Shinyanga kwenye Mkutano wa hadhara.
Kaimu Mwenyekiti wa BAWACHA Sharifu Suleiman akizungumza na Wananchi wa Shinyanga kwenye Mkutano wa hadhara.
John Heche akizungumza na Wananchi wa Shinyanga kwenye Mkutano wa hadhara.
Kaimu Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Serengeti Gimbi Masaba akizungumza na Wananchi wa Shinyanga kwenye Mkutano wa hadhara.
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe,(kushoto) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa Tundu Lissu kwenye Mkutano wa hadhara Mjini Shinyanga.
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu (kulia) akiwa na Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Zanzibar Salum Mwalimu.
Viongozi mbalimbali na wanachama wa Chadema mkoani Shinyanga wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara.
Viongozi mbalimbali na wanachama wa Chadema mkoani Shinyanga wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara.
Wananchi wa Shinyanga wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara.

Aliyekuwa Diwani wa CCM Manispaa ya Shinyanga Thomas na Kanda wa CCM wajiunga Rasmi CHADEMA.
Awali Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe akiwasili na Chopa kwenye Mkutano wa hadhara Mjini Shinyanga
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akiwasili eneo la Mkutano wa hadhara.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post